Posts

Showing posts from May 28, 2018

Nape atoa ujumbe mzito wa kumuaga Kinana

Image
Mbunge wa Mtama, na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Nape Nnauye amemaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu leo kuwa wataendelea kumuenzi na mbegu aliyopanda itaota. Nape ametoa ahadi hiyo kwa Kinana ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo Nape ameweka wazi kumtambua kinana kama mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma. "Pumzika rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi.  Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! Umepanda mbegu na itaota,"

MKE AMUUA MUMEWE KISA WIVU WA MAPENZI KAGERA

Image
Victoria Salvatory (58), mkazi wa kata ya Katoma, Kagera anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Salvatory Iteganira (62) kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amesema mauaji hayo yalitokea jana saa 6:00 mchana. Akizungumza leo Mei 28, Kamanda Ollomi amesema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mumewe kwa kitu kizito kichwani na kumsababishia jeraha lililovuja damu nyingi na hatimaye kifo. “Wanandoa hao wanadaiwa kuwa na ugomvi ambao chanzo chake tunaendelea kuchunguza; baada ya ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga mume wake kichwani kwa kitu kizito kilichosababisha jeraha lililovuja damu nyingi na kusababisha kifo chake,” amesema Ollomi. Kamanda huyo amewaasa wanandoa na wapenzi kutumia njia ya majadiliano, usuluhishi na sheria kutatua tofauti miongoni mwao badala ya kujichukulia sheria mikononi. Matukio ya hivi karibuni ya mauaji ya wanandoa ni pamoja na la Muuguzi mfawidhi msaidizi wa hos...

Maafisa wakuu wakamatwa kwa tuhuma za ufisadi.Kenya

Image
Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi. Hii inafuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni 9. Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na pia zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo NYS scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa uchunguzi wa Uhalifu George Kinoti. "Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana na sakata inayoendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara moja dhidi ya wite waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi. Washukiwa wengine kadhaa pia wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani katika kipindi cha saa 24, kulingana na afisa mmoja katik...

Kesiha Ateuliwa Mjumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM

Image
 MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya maarufu kwa jina la ‘Keisha’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (NEC) leo, Jumatatu, Mei 28, 2018.  Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kufuatia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Keisha ambaye aliwahi kutamba kwa ngoma yake ya uvuymilivu na nyingine, aliwapi pia kuwania Ubunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Dodoma na kushinda katika kura za maoni. Kabla ya uteuzi huo wa leo, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

BREAKING NEWS: KINANA ANG’ATUKA UKATIBU MKUU CCM

Image
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana ameng’atuka katika nafasi yake hiyo ndani ya CCM huku Halmashauri Kuu ya chama hicho ikiridhia ombi hilo rasmi. Hayo yamewekwa wazi na taarifa ilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 29, 2018 na kusema kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake. “Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika” , imesema taarifa hiyo. Kwa upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).

Mbowe Afunguka Kauli ya Mwisho ya Bilago Kabla ya Kifo

Image
MWENYEKITI wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema maneno ya mwisho aliyoambiwa na aliyekuwa Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, marehemu Kasuku Bilago kuwa alimwambia anahitaji msaada wa haraka wa matibabu. Akizungumza katika ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Bilago, Mbowe amesema wakati alipokuwa nje ya nchi, nchini Afrika Kusini Bilago alimtumia ujumbe kwamba hali yake kiafya si nzuri hivyo anahitaji msaada. “Nilipokuwa safarini nchini Afrika Kusini, mwalimu Bilago aliniambia ninaumwa hivyo naomba ushauri, nikawasiliana na bunge kuhusu taarifa yake ndipo walipomuamishia muhimbilli.Mwalimu aliliona hilo kwamba alikuwa anahitaji msaada wa haraka wa matibabu na kunitumia ujumbe nikiwa Afrika Kusini,” amesema Mbowe. Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa “Ndipo nilifunga safari Ijumaa, Jumamosi nilienda Muhimbili, nilimkuta hali yake imebadilika ghafla akakata kauli, nikaonana na madaktari ili wafanye juhudi za makusudi lakini walijaribu kwa muda wa nusu saa...

Mkutano Mkuu wa CCM Mambo Moto

Image
MASIKIO ya wengi yameelekezwa kwenye mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika leo (Jumatatu) na kesho jijini Dar es Salaam, ambapo vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) vikitarajiwa kuwasha moto wa uamuzi mgumu unaotajwa kuwa ni nadra kutokea ndani ya chama hicho tawala. Tangu mkutano huo utangazwe ukifuatiwa na kutolewa kwa ripoti ya ya uchunguzi wa mali za CCM nchi nzima kumekuwepo na habari nyingi zinazohusisha uwezekano wa vikao hivyo kutoka na maazimio mazito, hata hivyo, chanzo kutoka ndani ya chama hicho kimeliambia Ijumaa Wikienda kuwa, agenda zake zitaleta mwangwi miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla. “Ni vikao vizito vitakavyoamua mambo mazito yenye faida kwa chama chetu, siwezi kusema ni yepi lakini tega masikio utasikia, CCM ni chama kikongwe na makini lazima mikutano yake hasa ya kitaifa iamue mambo makini .“Huwezi kuwa na chama kama hiki, kinachoshika dola halafu kiwe na mikutano ya kitotokitoto, wanaosema kitakuwa moto ni ...

Kijana aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi Serikalini

Image
Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito. Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa. Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha, Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa. Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possi...

TAJIRI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA, BASTOLA – DAR

Image
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewatia mbaroni watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, Ayoub Kiboko na mkewe, Pilli Kiboko, Mei 23, saa 8 usiku wakiwa nyumbani kwao eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam baada ya kuwasaka kwa muda mrefu. Kiboko ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara waliotajwa katika barua za Watanzania waliofungwa Hong Kong, ni maarufu ndani na nje ya nchi na anadaiwa kumiliki hoteli kubwa zaidi ya 10 pamoja nyumba za kifahari katika maeneo mbalimbali hapa jijini. Barua hizo zililetwa nchini Desemba 2014 na Kasisi John Wotherspoon anayesaidia wafungwa katika magereza ya Hong Kong na China na baada ya Watanzania hao kuandika barua hizo wakiwaasa wengine wasifanye biashara hiyo huku wakiwataja wafanyabiashara waliowabebesha dawa hizo za kulevya akiwamo Kiboko. Kamishna wa Operesheni DCEA, Frederick Milanzi alisema katika msako uliofanywa nyumbani kwake usiku wa manane, walimkamata Kiboko akiwa na dawa za kulevya...

RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP HII HAPA KUNA ASILIMIA 90 SIMBA NA YANGA KUKUTANA NUSU FAINALI

Image
Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajia kuanza Juni 3 ,2018 kwa timu nane kushirikia ambazo zinadhaminiwa na Kampuni hiyo kubashiri Matokeo Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda kucheza na Everton nchini Uingereza. Watani wa Jadi Simba na Yanga kuna uwezekano Mkubwa wakakutana Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Derby ya Mashemeji huenda ikatokea tena kama walivyokutana kwenye Fainali ya Msimu uliopita walipocheza uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Ratiba Kamili ni: Robo Fainali 03/06/2018 13:00 Kakamega Home Boys vs Yanga sc 15:15 Gor Mahia vs JKU 04/06/2018 15:00 Kariobangi Sharks vs Simba Sc 05/06/2018 15:00 AFC Leopards vs Singida United Nusu Fainali 07/06/2018 13:00 Winner (Gor Mahia vs JKU) vs (AFC Leorpard s vs Singida Utd) 15:15 Winner (Kakamega Home Boys vs Yanga Sc) vs ( Kariobangi Sharks vs Simba Sc) Mshindi wa tatu 10/06/2018 12:00 Loser Nusu Fainali Fainali 10/06/2018 ...