Posts

Showing posts from July 27, 2018

BETHIDEI YA TIFFAH KUFURU

Image
DAR ES SALAAM: Maandalizi ya pati ya kuzaliwa (birthday) ya bintiye ambaye ndiye uzao wake wa kwanza, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ (3), yamemfanya baba’ke ambaye ni staa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa kiapo kizito kuwa itakuwa ni shughuli ya kufuru, Risasi Jumamosi linakupa exclussive. Agosti 6, mwaka huu, Tiffah atatimiza umri wa miaka mitatu tangu alipozaliwa Agosti 6, 2015, lakini sherehe hiyo imesogezwa mbele ambapo sasa itafanyika Agosti 17 hadi Agosti 20, mwaka huu. DIAMOND NA RISASI JUMAMOSI Akizungumza na Risasi Jumamosi juu ya pati hiyo ya Tiffah ya kutimiza umri wa miaka mitatu, Diamond alisema kuwa, yupo tayari kufilisika, lakini ahakikishe mwanaye huyo ana furaha kwa kumfanyia pati hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria. “Nimepanga iwe sherehe kubwa sana, acha nifilisike, lakini mwanangu afurahi,” ndivyo alivyoanza Diamond kwenye mahojiano hayo maalum na Risasi Jumamosi na kuongeza: “Nipo tayari kutumia sehemu ya pesa za

TAGCO NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZAPONGEZWA KWA UTENDAJI

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza kuhusu namna Halmashuri hiyo ilivyojipanga katika kuimarisha mawasiliano ya kikakati hasa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea  Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao. Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamoja katika

WAZEE WA NITUMIE PESA KWA NAMBA HII’… WANASWA

Image
I RINGA: Yawezekana wewe ni kati ya watu ambao walishawahi kutumiwa meseji za kitapeli kutoka kwa watu hao (pichani) ambao huandika hivi; ‘ile pesa nitumie kwenye namba hii, jina litatokea…, simu yangu ina tatizo’. Kama jibu ni ndiyo basi habari ikufikie kwamba, watuhumiwa wengine wapatao saba wa utapeli huo hivi karibuni wamenaswa mkoani Iringa baada ya kuwaliza watu wengi kwa muda mrefu. Watu hao wamekuwa wakiwatumia watu meseji na kuwaelekeza kuwa watume pesa, mazingira ambayo baadhi huenda walikuwa na watu ambao ilikuwa wawatumie pesa hivyo hutuma na kujikuta wametuma kwa matapeli hao. POLISI WATANGAZA VITA Kufuatia kushamiri kwa utapeli huo katika mikoa mbalimbali, jeshi la polisi kupitia kwa makamanda wa mikoa hivi karibuni lilitangaza vita dhidi ya uhalifu huo na kufanikiwa kuwanasa baadhi ya watu huku tahadhari ikitolewa kwa wananchi kuwa makini wanapokumbana na meseji za aina hiyo. WALIONASWA IRINGA Mbali na wale 15 wa hivi karibuni waliokamatw

MWANAMKE KUKOSA MSISIMKO WA TENDO LA NDOA

Image
T ATIZO hili la mwanamke kukosa msisimko wa tendo la ndoa kitaalamu tunaita ‘Female Sexual arousal disorder’. Mwanamke akiwa na hali hii huwa hajihisi hamu wala haja ya kuhitaji tendo hilo na wakati mwingine huona kama usumbufu endapo atakuwa katika mahusiano. Mwanamke wa aina hii kama yupo mwenyewe au ‘single’ haoni umuhimu wa kuwa na mpenzi au mwenza na hasa kama anajimudu kiuchumi. Wapo baadhi ya wanawake wenye hali hii ambao hawana watoto au wengine wanamtoto mmoja au zaidi na aidha wameachana na wenza wao au wenza wao walishafariki. Msisimko hupatikana baada ya hamu ya tendo la kujamiiana kuwa juu ya kiwango na kusababisha mabadiliko mwilini na kusaidia mwili uwetayari kwa tendo. Hali ya msisimko kwa mwanamke haina tofauti na hali ya mwanaume kusimamisha uume wake. Mwanamke aliyepoteza msisimko huwa hajisikii chochote wakati wa ’ Romance’ au maandalizi ya tendo la ndoa, wengine huwa hawapati hamu na wengine hupata hamu kwa kiasi kidogo lakini hawapati mguso au

Diamond azuiwa na Basata kwenda kufanya shoo nje

Image
BARAZA la  Sanaa Tanzania (BASATA) leo limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali. Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Onesmo Mabuye alipokuwa akizungumza na TBC, kuhusiana na sintofahamu hiyo kuwa ni kutokana na msanii huyo kukosakibali cha Basata. BASATA wamesema kwa sasa hivi kuna utaratibu mpya ni kuwa msanii akitaka kwenda kufanya shoo nje ya nchi ni lazima apitie kwa BASATA wampe kibali na kisha akirudi pia anatakiwa kuripoti kwao BASATA wamesema kumzuia Diamond wanataka iwe fundisho kwa wasanii wengine ili wanapoenda nje ya nchi wafuate taratibu zilizowekwa.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU AGAWA BAISKELI KWA WALEMAVU

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge wanaoishi katika mazingira magumu. Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,Nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga. Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa

Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika

Image
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaz

Zari Awapiga Stop Wema, Aunt: Sitaki Kunichafulia Nyumba, Kaeni Hukohuko

Image
IKIWA ni saa chache baada ya mwanamuziki Diamond Platnumz kualika watu takribani 50 kuuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mtoto wake  Tiffah, mzazi mwenzake, Zari Hassan amepiga marufuku ugeni huo. Jana wakati wa sherehe ya kufikisha siku 40 ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema, Diamond alialika wanakamati zaidi ya 10 kuhudhuria sherehe hiyo ya Tiffah, Sauzi hukuakisema atalipia tiketi za watu 30 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe na kuwalipia watoto 10 na wazazi wao. Hata hivyo, Zari amemjibu kupitia mtandao wa Instagram aliandika kuwa hautaki ugeni huo akihofia kuchafuliwa nyumba yake:  “Sitaki kunichafulia nyumba kaeni hukohuko.” Miongoni mwa wanakamati walioalikwa ni Wema Sepetu ambaye amewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz na mwigizaji Aunty Ezekiel. Tiffah ambaye jina lake halisi Latiffah alizaliwa Agosti 6, 2015. Hata hivyo sherehe za kuzaliwa binti huyo zitafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 17- 19 mwaka huu.