Posts

Showing posts from October 25, 2017

Hali Ilivyo Jijini Nairobi… Raila Odinga Vs Jeshi la Polisi

Image
POLISI Kikosi cha Kuzuia Ghasia wamefunga eneo lote la viwanja vya Uhuru Park jijini kabla ya mkutano ulioandaliwa na muungano wa National Super Alliance (NASA) kwa ajili ya kiongozi wake mkuu Raila Odinga kutoa tamko zito kuhusu mchaguzi wa marudio kesho. Maofisa wa polisi wakiwa katika sare zao wamesambazwa muda mfupi baada ya uongozi wa Kaunti ya Jiji la Nairobi kumwandikia kamanda wa Japhet Koome akipinga uwanja huo kutumiwa na Nasa. Gavana wa Nairobi Mike Sonko amemtaka kamanda Koome kuhakikisha eneo hilo linakuwa na usalama akihofia unaweza kutumika kwa “mkutano ambao haujaruhusiwa”. “Nimefahamishwa kwamba viongozi wa National Super Alliance (Nasa) wanapanga kutumia viwanja vya Uhuru Park kwa mkutano wa kisiasa leo. Hata hivyo, rekodi za uongozi wa jiji zinaonyesha hawajafuata utaratibu wa kupata kibali kwa ajili ya mkutano huo,” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Kamanda Koome. Sonko amesema hakuna mkutano utakaoruhusiwa kwenye viwanja hivyo bila ya ri...

Zitto Kabwe: Nipo Tayari Kuwajibika Rais Akitekeleza Ombi Hili

Image
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa atakuwa tayari kuwajibika endapo Rais Dkt John Magufuli ataruhusu uchunguzi huru wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mapato ya serikali yatakutwa hayajashuka kama ambavyo amekuwa akisema. Zitto ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Rais Magufuli alipokanusha madai yake akivitaka vyombo vya dola kuwafikisha mahakamani  watu wanaobadilisha takwimu za serikali wakiwamo wanaosema kuwa mapato ya serikali yameshuka wakati sio kweli ili wakathibitishe kauli yao. “Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma. Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA.” Katika taarifa yake, Zitto amezidi kusimamia msimamo wake akidai kuwa taarifa za mapato za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni za uongo, na kwamba,  taarifa ya kupikwa kwa takwi...

Mbunge ashtakiwa kwa kukojoa hadharani Uganda

Image
Mahakama moja nchini Uganda imempiga faini ya Shilingi 40,000 za Uganda mbunge mmoja nchini humo kwa makosa ya kukojoa hadharani. kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua siku ya Jumanne aliwasili mbele ya mahakama ya mji wa Kampala na kushtakiwa kwa kukojoa katika ukuta wa jumba la wizara ya fedha. Alikiri kufanya makosa hayo na akaachiliwa baada ya kulipa faini. Kwa mujibu wa gazeti hilo Kiongozi wa mashtaka aliambia mahakama kwamba mbunge huyo alifanya makosa hayo mwezi Septemba 25 mwaka huu katika barabara ya Kyaggwe mjini Kampala. Upande wa mashtaka ulisema kuwa vitendo vya mbunge huyo vilikuwa kinyume na sheria za baraza la manispaa ya Kampala za 2016. Kukiri kwake kunajiri baada picha kadhaa za yeye akikojoakando kando ya barabara kusambaa katika mitandao ya kijam

Zijue sababu zinazopelekea wapenzi wengi kuchokana mapema

Image
Hivi uliwahi kujiuliza hivi ni kwanini baadhi ya mahusiano ya kimapenzi hufa mapema, kama si kufa basi kushuka kwa mahusiano hayo? Moja kati ya sababu ambayo husababaisha kufa kwa mahusiano ni ile tabia ya kuchokana mapema katika mahusiano na moja kati ya sababu kubwa ambayo hupelekea kuchokana mapema ni: 1. Mazungumzo Mazungumzo ni njia muhimu ya kujenga ndoa na kuiimarisha , aidha ni njia ya mkato ya kuchokana na kuchukiana. Mwanamke ambaye hajui wakati gani aseme nini na wakati gani asiseme, hujikuta katika wakati mgumu ndani ya ndoa yake. Kwa mfano: Mwanamke ambaye kila anapoongea na mume wake huanza mazungumzo yake na matatizo na lawama humfanya mumewe awe na woga kila anaposikia sauti yake, na kuiona nyumba chungu, kwa sababu hakuna binadamu anayependa kusikia matatizo tu wakati wote Mwanamke wa aina hii huwa anamsubiri mumewe kwa hamu kubwa, na anapofika tu na kabla hata ya kupata rizki, anaanza kumsomea orodha ya matatizo; watoto wamerudishwa shule, karo h...