MZEE WA UPAKO NAE AFUNGUA HAYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake. Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano. “Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile ...