Posts

Showing posts from January 31, 2017

UFAULU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016 WAPAA

Image
  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016. Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26. Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015. Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.

BREAKING NEWS : ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

Image
THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA. English ... NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania. BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YOTE HAPA