Posts

Showing posts from April 2, 2016

ZIFAHAMU FAIDA KUMI ZA MMEA WA ALOE VERA KWA BINADAMU...

Image
                                                                  mmea wa aloe vera ni mmoja ya mimea ambayo imejizoelea umaarufu miaka hii ya karibuni  baada ya kuonyesha kutibu na kuzuia aina mbalimbali za magonjwa, lakini pia kurefusha maisha na kupunguza makali ya magonjwa yasiyopona kama kisukari, presha, magonjwa ya moyo, pumu, kifafa, ukimwi na mengine mengi, lakini mmea huu ulikua ukitumika tangu miaka ya zamani sana na watu waliishi miaka mingi wakiwa na nguvu na akili kupitia mmea huu. kwa faida za mmea huu ni bora kumiliki hata bidhaa moja tu ambayo utakua unaitumia siku zote za maisha yako ili kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa hatarishi..kwa sasa kampuni ya forever living product ndio inaongoza kwa mauzo hayo duniani, ikiwa imetapakaa zaidi ya nchi 150.hapa tanzania ikiwa  im...

Mwanamuziki Lady Jaydee Azungumzia Msanii wa Kiume Anaemfikiria Sasa Kushirikiana Naye

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi. Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue. "Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue" alisisitiza Lady Jaydee Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa ...

Shamsa: Nusura niharibike ubongo kwa kipigo

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. Stori: Imelda Mtema Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki. “Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa

Fina Mango na Masoud Kipanya waongezeka katika timu ya Power Breakfast ya Clouds Fm

Image
Siku kadhaa zilizopita katika mitandao ya kijamii zilisambaa habari za kuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm, Gerrard Hando na Paul James (PJ) wameondoka katika redio hiyo. Katika kipindi hicho cha Power Breakfast leo Ijumaa, Aprili 1 zimesikika sauti mpya katika kipindi hicho ambapo ni Fina Mango na Masoud Kipanya ambao wamesikika katika kipengele cha kuperuzi na kudadisi ambacho kinahusika na kupitia magazeti ya siku husika. Baada ya kuongezeka kwa watangazaji hao, inaonyesha dhahiri kuwa Gerrard Hando na PJ watakuwa wameondoka katika kituo hicho baada ya kudumu kwa kipindi kirefu ambapo mikataba yao ilimalizika jana Machi, 31.

MAKONDA AWAGEUKIA BODABODA WA DSM.AWAAHIDI PIKPIK KWA SH.3,500 KWA SIKU,KUINGIA POSTA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo. Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao. Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon (Maktaba) Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa. Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana. Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia ...

SAKATA LA WASTARA MAPYA YAIBUKA,MBUNGE ASEMA AMELOGWA NA WASTARA,AJIBU MAPIGO,AELEZA MAZITO

Image
  Makubwa! Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga, twende na Risasi Jumamosi. Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele. Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili. Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?” ILIKUWA HIVI Risasi Jumamosi: (baada ya kujitambulisha na salamu) “mheshimiwa tunataka kujua nini kinaendelea kati yako na mkeo Wastara?” Mume: “Kuhusu nini?” Risasi Jumamosi: “Kuna madai kwamba, ...