Machafuko Yanayoendelea Kwenye Kasri ya Mfalme Uganda, Mwandishi wa KTN Akamatwa
Mwandishi wa habari wa runinga ya KTN ya nchini Kenya, Joy Doreen Biira amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama nchini Uganda jana Jumapili usiku. Vyombo vya habari zinasema Bi Biira alikamatwa pamoja na wengine watano kwa tuhuma za kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa wa usalama katika kasri la mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii. Wanahabari na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wametoa wito kwa serikali kumwachilia huru. Hash Tag #FreeJoyDoreen (Mwachilie huru Doreen) kinavuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya. Wanajeshi na polisi walivamia kasri hilo la Mfalme Charles Wesley Mumbere Jumapili. Walinzi wake 46 waliuawa kwa mujibu wa polisi, na wengine 139 wakakamatwa. Mfalme huyo alikamatwa pia na kuzuiliwa makao makuu ya polisi ya wilaya ya Kasese kabla ya kuhamishiwa mjini Kampala. Gazeti la linalomilikiwa na Kampuni binafsi ya Monitor nchini humo linasema mfalme huyo anatarajiwa kukutana