SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine yameibuka. Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa. Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena. “Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo. Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake. “Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa n...