Muigizaji wa Siri za Familia apata ajali
Luwi Cappelo Muigizaji wa filamu Luwi Cappelo wa nchini Kenya ambaye ameigiza tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na East Africa Television, amepata ajali ya gari na kulazwa hospitali ya Pandya mjini Mombasa Kenya, katika chumba cha wa wagonjwa Mahututi. Mkurugenzi wa Jasson Production ambao ndio watengenezaji wa tamthilia ya Siri za Familia, Bw. Sanctus Mtsimbe, amesema kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Lui akiwa njiani kuelekea Mombasa kwenye harusi huku akiwa na wenzake, lakini baadaye alipata taarifa za ajali hiyo. Hata hivyo Siri za Familia zimetoa taarifa rasmi ya ajali hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram, ukiandika...”Tumepata taarifa kupitia wenzetu wa Nairobi kuwa siku ya Jumapili saa 8 alfajiri, muigizaji wetu wa Siri za Familia msimu wa 4 kutoka Kenya Luwi na rafiki zake watatu, walipata ajali katika barabara ya Mombasa - Malindi wakiwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi. Luwi alikuwa amekaa nyuma na aliumia, kwa sasa Luwi amelazwa Hospita...