Jinsi ya Kuangalia kama Simu ni Feki
Hivi karibuni zilisambaa taarifa kwamba simu feki zote nchini Tanzania zitazimwa ifikapo mwezi Juni mwaka 2016, makala hii itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki ama la. Hatukuweza kuthibisha moja kwa moja kwamba kweli simu zitazimwa mwezi Juni lakini tumejiridhisha kuwa kutakuwa na hatua dhidi ya wanaomiliki simu feki pindi itakapofika tarehe hiyo. Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia. Jinsi ya angalia IMEI namba Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15. Nakili namba hizo pembeni. Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa kupi...