Vilio vya Mastaa kwa Wanafunzi Waliokufa Arusha
M AJONZI yamegubika nchi nzima kufuatia tukio la kihistoria la ajali ya basi lililosababisha vifo vya wanafunzi 33, walimu wawili na dereva iliyotokea Karatu mkoani Arusha. Taarifa zinasema kuwa basi hilo aina Toyota Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi, walimu na dereva ambalo ni mali ya Shule ya Lucky Vincent liliacha njia na kutumbukia katika Mto Marera uliyopo kilometa 25 kutoka kwenye geti la Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Mbali na ajali hiyo kuwagusa wengi ndani na nje ya nchi, mastaa kutoka kwenye tasnia mbalimbali nchini wameibuka na kuzungumza na Wikenda, wakiweka wazi hisia zao za namna walivyoguswa na ajali hiyo. Wasikie; PROFESA JAY: Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi. Kiukweli hili ni pigo kubwa sana kwa taifa letu, natoa pole sana kwa ndugu, jamaa wa marehemu na viongozi wote wa Mkoa wa Arusha kwa msiba huu mkubwa. Kwa mara nyingine tena kama taifa tunapoteza watoto wetu kwa idadi kubwa sana ambao wangeweza kuja kuwa hazina kubwa kwa ...