MAMBO KUMI (10)YA KUZINGATIA WAKATI WA UJAUZITO KWA AJILI YA AFYA YA MAMA NA MTOTO.
1.Punguza matumizi ya vyakula vyenye “caffeine” Kama vile chai, kahawa na soda za cola huweza kusababisha mimba kuharibika au kutoka. 2. Kula vizuri chakula chenye mlo kamili na aina mbalimbali za matunda ili kujenga afya yako na ya mtoto. 3. Pata muda wa kutosha wa kupumzika ili kutuliza mwili na akili kwa afya yako na ya mtoto. 4. Fanya mazoezi madogo madogo ya viungo kama kutembea, kuogelea na yoga mara kwa mara 5. Kunywa dawa za kuongeza vitamini mwilini “Pregnancy vitamin” endapo huna uwezo wa kula chakula chenye mlo kamili lakini isiwe mbadala wa chakula 6. Acha kuvuta sigara kama ni mtumiaji kwani husababisha madhara kwako na pia mimba kutoka, kuzaa mtoto kabla ya siku kutimia na mtoto kufariki akiwa tumboni. 7. Acha kunywa pombe kwani humfikia mtoto kupitia mirija ya damu na “placenta” kama ukishindwa kabisa punguza kwa kiasi kikubwa. 8. Baada ya kugundua tu una mimba muone mkunga kwaajili ya maelekezo na ratiba ya jinsi ya kuhudhuria kliniki. 9