Posts

Showing posts from November 9, 2018

Waziri Kabudi akwepa kujibu swali la Zitto Kabwe

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe. Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi amekwepa kujibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kutokana na kile alichokisema kuwa ni mtego ambao unaweza kuliingiza taifa kwenye hasara dhidi ya kesi zake za kimataifa. Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa 13 Zitto Kabwe amehoji juu kwanini serikali ishitakiwe wakati imekuwa kwenye mazungumzo na kampuni tanzu za ACACIA pamoja na kuhoji kwanini serikali imefungua kesi dhidi ya kampuni za madini juu ya kukwepa kodi. Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi akijibu swali amesema maswali ya mbunge huyo asingeweza kuyajibu kwasababu yataathiri ushahidi wa serikali kwenye kesi zake zinazoendelea. "Masuala yote ya uliyoyasema yaliyo kwenye mahakama za kitaifa na kimataifa ni yanaendelea, nataka niwaambie mtego huo uwe wa bahati mbaya, wa kutumwa au bahati ambaya sitauingia kamwe kwa sab...

Diamond kumfungulia Hawa biashara baada ya kuona afya yake inaimarika

Image
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefurahishwa na habari zilizoenea za kuwa Hawa anaendelea vizuri baada ya kumgharamia matibabu yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandiaka hivi:-

BREAKING: Mabehewa ya Treni Yaanguka Morogoro

Image
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, mabehewa mawili ya treni ya mizigo ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) yaliyokuwa yamebeba kijiko yameanguka katika eneo la Mazimbu mkoani Morogoro, wakati likitoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma leo Ijumaa, Novemba 9, 2018. Aidha, Hakuna majeruhi wala kifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo. Endelea kufuatia taarifa zetu.

Mobetto Amtambulisha Mrithi wa Penzi la Diamond

Image
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Hamissa Mobetto amevunja ukimya na kuamua kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kuachana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa amepost picha akiwa na mwanaume huyo ambaye jina lake halijajulikana mpaka sasa hivi na kisha akaandika ; “Roho Mkalia Moyo” Ikumbukwe kuwa Hamisa kwa sasa yuko nchini Marekani katika tour yake akiwa na msanii Christian Bella. You May Like