Yanga yamuacha Kessy
Mchezaji wa Yanga, Hassan Kessy. Wilbert Molandi, Dar es Salaam MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga, asubuhi ya kesho Jumamosi utaondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya kukipiga na Medeama ya nchini humo huku wakiwaacha mabeki wao, Hassan Kessy na Mtogo, Vincent Bossou. Yanga itarudiana na Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 16, mwaka huu. Chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, Yanga inatakiwa kushinda kwenye mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kucheza Nusu Fainali ya michuano hiyo, kinyume na hapo hali ya mambo inaweza kuwa mbaya na yawezekana wakawa wamefuta ndoto za kusonga mbele. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema msafara wao unatarajiwa kuwa na watu 30, kati ya hao, wachezaji ni 21 na viongozi tisa. Amesema msafara huo unatarajiwa kuondoka saa moja asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JN...