Posts

Showing posts from March 24, 2018

Marekani: FBI Aliyetambua Shamulio la Osama Afariki kwa Sumu

Image
SHIRIKA la Uchunguzi la Marekani (FBI) limesema limempoteza mwanamama mmoja ambaye ni miongoni mwa waliotambua shambilizi la kigaidi la Septemba 11, 2001 lililofanywa na Osama BinLaden, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48. Melissa S. Morrow alifariki juzi Alhamisi akiwa na miaka 48 kwa kansa ya ubongo huku ikielezwa kuwa, huenda kifo chake kilisababishwa na kuwekewa vitu vyenye sumu (kemikali). Mtaalam huyo wa uchunguzi, amefanya kazi ndani ya FBI kwa miaka 22, na wakati umauti unamfika alikuwa ana siku chache tangu ahamishiwe katika kituo kipya cha kazi, Kansas City. Taarifa ya FBI imeeleza kuwa, Morrow alikuwa amejitoa kwa kiasi kikubwa kulitumikia taifa lake kwa kuchunguza na kubaini ukweli wa shambulio la Spetemba 11, katika Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon,. Inadaiwa mama huyo baadaye alikutwa kwenye  ghala lenye sumu mwaka 2013 jambo lilliloplekea kuzorota wa kwa fya yake  licha ya kutibiwa kwa zaidi ya wiki 10 huku akikusanya taarif

Waziri Mkuu Majaliwa aridhishwa na ujenzi wa Terminal III

Image
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake. Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka na kuwa na. Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi. “Serikali imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.” Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iring