Posts

Showing posts from April 30, 2015

ISIS WAENDELEA KUFANYA MAUAJI YA KUTISHA HUKO SYRIA NA IRAQ

Image
Mmoja wa watuhumiwa wa uchawi akiwa tayari kuchinjwa na Kundi la ISIS huko Raqqa, Syria. Mtuhumiwa mwingine wa uchawi naye akiwa tayari kuchinjwa na ISIS. Mpiganaji wa ISIS akinyanyua tofali la zege kumpiga mmoja wa wanaume waliokamatwa kwa kuua wanawake. Adhabu ya kuwapiga mawe wanaume waliokamatwa kwa mauaji ya wanawake watatu ikiendelea huko Iraq Kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao na mmoja wa wapiganaji wa ISIS. Picha ya mashoga wawili waliowekwa mitandaoni na Kundi la ISIS kabla ya kuwapia mawe hadi kufa. Mashoga hao wakipigwa mawe hadi kufa na wapiganaji wa ISIS huko Syria.WAPIGANAJI wa ISIS wamefanya mauaji ya kutisha kwa mateka wawili wa kiume waliotuhumiwa kuwaua kwa kuwapiga virungu wanawake watatu huko nchini Iraq. ISIS waliwapiga watuhumiwa hao kwa matofali ya zege kichwani hadi kufa ikiwa ni adhabu kwa kitendo chao cha kuiba na kuwaua wanawake watatu. Tukio hilo limefanyika katika Mkoa wa Nineveh huko kaskazini mwa Iraq. Katika tukio lingin

UKAWA: UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 LAZIMA, KIKWETE ASIONGEZEWE MUDA, KURA YA MAONI BAADAE

Image
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba (kushoto)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa (kulia). VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo vimetoa msimamo wao juu ya njama za kuahirisha Uchaguzi Mkuu unaotakiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Ukawa imesisistiza kwamba kuahirisha kwa Uchaguzi Mkuu huo ni sawa na kumuongezea Rais Jakaya Kikwete na Chama chake cha CCM muda wa kuendelea kuitawala Tanzania. Ukawa imesema jaribio lolote la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa kisingizio chochote kile litakuwa ni kinyume na katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Msimamo wa UKAWA unafuatia kumalizika kwa kikao cha Viongozi Wakuu wa Vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) jijini Dar kati ya tarehe 28 na 29 Aprili mwaka huu. Akieleza msima

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI

Image
Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango, kutoka shoto ni Bi. Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba, Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance. Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group, kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na  Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group. Bi Fauzia Kullane.  Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba, kwenye hafla fupi ya utoaji

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA DANGOTE

Image
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. Watatu kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake jijini Dar es salaam April 30, 2015. Kushoto kwake ni balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kushoto) na  balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu (kulia) baada ya mazungumzo yao  ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. (picha na Ofisi ya