Posts

Showing posts from June 15, 2016

MANENO MUME ALIYOMWAMBIA MKE WAKE USIKU BAADA YA SHEREHE YA HARUSI YAO.

Image
   "Mke wangu, watu wote wameenda nyumbani kwao , mziki umezimwa, shamrashamra zimeisha. Harusi yetu ilikua nzuri mno ila sasa imepita. Tumemaliza harusi sasa ni muda wa kujenga familia yetu. Tuliobaki baada ya harusi hii ni mimi na wewe tu peke yetu. Hatma ya kesho huanza leo. Maisha yetu sasa sio kama ya nyuma ... . Nakumbuka kuna kipindi ulivaa gauni jekundu, lilikupendeza sana, siku ile nlitaman kukugusa, tulikua kwenye maonyesho ya sinema nilikua na shauku kubwa sana kwako. Nilitamani japo kukusogeza upande wa chooni ili nikakubusu tu ila haikuwezekana. Niliumia sana moyoni. Ila sasa wajua nini siri ya furaha yangu? Jibu la siri ya furaha yangu ni kuwa sasa nimekupata, niko na wewe pamoja milele, naweza sasa kukubusu kila siku. Kabla sijakuvua nguo na kufanya mapenzi na wewe kwanza ngoja nikuambie vitu vichache vya muhimu mno......... Sina cha kukuficha, kuanzia leo simu yangu waeza kuitumia kama yako pia waeza tumia account na profile zangu Facebook, whatsapp na...

NJIA RAHISI KUSOMA QUR-AN YOTE KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Image
  Qur’an ina juzuu thelathini sawa na siku thelathini za mwezi, hivyo kwa kusoma juzuu moja kila siku inatosha kutimiza Qur’an yote kwa mwezi, ikumbukwe pia Qur’an (mas’haf) ina kurasa kati ya 604–612. Inahitaji kusoma kurasa ishirini kwa siku kwa muda wa siku thelathini kumaliza msahafu mzima. Siku moja ina swala tano, zikigawiwa kurasa ishirini kwa swala tano zinapatikanaka kurasa nne katika kila swala. zikigawiwa kurasa nne kwa mbili, yaani itakuwa kurasa mbili kabla ya swala na mbili baada ya swala, ni kiasi chepesi kwa mtu kuisoma Qur’an nzima ndani ya mwezi. Kwa wale ambao hawana muda wa kusoma kurasa nne kila swala, hebu tujaribu hii. Tusome kurasa saba baada ya swala ya sub’hi (alfajir), saba baada ya swala ya laasiri na saba baada ya taraweeh (swala ya Isha). Hivyo itakuwa saba mara tatu ambayo ni sawa na 21. 21 mara siku thelathini ni 630 yaani msahafu na zaidi. Ikumbukwe tabia hujenga mazoea, hebu chagua hesabu moja na uanze nayo mazoezi katika maisha, Mwisho ...

Usome Hapa Waraka wa Edward Lowassa kwa IGP Mangu

Image
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa. Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Salaam, Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako. Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwana kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa. Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jeneraliwa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa namaandamano ya vyama vya upinzani. Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko njeya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema nataifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizolako hilo. IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanyahivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoakuwa...

Mbunge wa Ukonga Ashinda Kesi ya Uchaguzi

Image
    Mbunge wa Jimbo la Ukonga (Chadema), Mwita Waitara (kulia) akitoka mahakamani. (Picha na Maktaba). Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara leo ameshinda kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jerry Silaa. Hukumu hiyo imetolewa leo muda mfupi uliopita na Jaji Fatma Msengi wa Mahakama Kuu ya Dar es Salaam.

Wolper nusura apigwe risasi ‘sheli’

Image
Jacqueline Wolper. NA MUSA MATEJA, RISASI MCHANGANYIKO DAR ES SALAAM: Chupuchupu! Mwanadada anayeng’ara kunako tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati almanusra apigwe risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa timbwili zito eneo hilo, Risasi Mchanganyiko linakupa mkasa mzima. Tukio hilo la aina yake, lilijiri mishale ya saa tano usiku wa Juni 12, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Wolper alinusurika kupigwa risasi na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta baada ya kutokea hali ya sintofahamu kati yake na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho. “Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale sheli (Sheli ni neno lililozoeleka likimaanisha kituo cha mafuta, lakini ukweli ni kuwa jina hilo ni la kampuni ya mafuta yenye makao makuu yake Nchini Marekani) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab ...

ANGALIA RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND MSIMU 2016/2017

Image
  Kama wewe ni shabiki la Ligi Kuu England ratiba ya Ligi kwa ajili ya msimu wa 2016/2017 imetoka, rasmi sasa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 itaanza kuchezwa rasmi Jumamosi ya August 13 2016, bingwa mtetezi wa Leicester City ataanza kwa kucheza na Hull City. Unaweza bonyeza  HAPA  kupata ratiba yote. A

Ukweli afya ya Spika Job Ndugai

Image
Spika wa Bunge, Job Ndugai. KUFUATIA uvumi wa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii juu ya kufariki dunia kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Risasi Mchanganyiko limetafuta na kufanikiwa kupata ukweli juu ya afya ya kiongozi huyo mkuu wa wabunge Tanzania. Awali, kulikuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii, ikitoa madai hayo, hasa kutokana na kutoonekana kwa muda mrefu kwa Spika akiongoza vikao vya Bunge vinavyoendelea kujadili bajeti kuu ya serikali mjini Dodoma. Kutotolewa kwa maendeleo ya afya yake ndilo jambo linalowafanya wengi kuziamini taarifa hizo za mitandaoni na hivyo kupiga simu chumba cha habari kutaka kujua uhakika wake hasa kwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Spika kwenda nchini humo kuangaliwa afya yake. Gazeti hili lilimtafuta Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah ili kupata ufafanuzi wa taarifa za mitandao zilizokuwa zikitembea juzi (Jumatatu) kuwa mbunge huyo wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma amefariki, lakini simu yake haikupo-kelewa. Lakini Kaimu Katibu wa...