Posts

Showing posts from January 26, 2017

JKCI KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI AFRIKA WA NCHINI MAREKANI WATOA HUDUMA YA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA

Image
Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Kulia ni Dkt. Peter Kisenge, akifuatiwa na Dkt. Peter O’brien na kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau. Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Madaktari Afrika wa nchini Marekani Dkt. Peter O’brien na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari Afrika wa nchini Mare...

ASKARI WAUA WATU 4 ARUSHA

Image
WATU wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa ulinzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) huku mwanafunzi wa darasa la tatu anayesoma Shule ya Msingi Lemingori iliyopo Oldonyosambu wilayani Arumeru, Isaya Thomas (13) akiwa miongoni mwa majeruhi wa shambulio lililofanywa na askari hao. Kutokana na tukio hilo, Polisi inawashikilia askari sita wa Suma JKT kwa uchunguzi dhidi ya tukio hilo lililotokea Kijiji cha Kandaskirieti Kata ya Oldonyosambu Tarafa ya Mukulati huku miili ya watu wanne waliokufa kutokana na shambulio hilo, ikiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo akizungumzia tukio hilo, alisema juzi saa 11 jioni katika Kijiji cha Kandaskirieti, watu wanne walikufa baada ya kupigwa risasi na askari wa Suma JKT. Alisema taarifa za awali zimebaini kuwa askari hao wa Suma JKT ambao ni walinzi wa shamba la miti la serikali la Meru Usa Plant, walianza kufanya operes...