Posts

Showing posts from October 19, 2015

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI MPYA,

Image
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayotajwa kuwa kubwa katika Afrika. Akihutubia katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Massawe afuatilie barua yake rasmi ya uteuzi. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Februari mwaka huu, huku akitajwa kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. Kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam. Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili. Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamisi ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya kuboresha ufanisi katika