Posts

Showing posts from July 24, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 24.07.2014

Image
 

ANGALIA PICHA KIJANA "ANG'OLEWA" MENO 232

Image
Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba. Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye t aya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai. Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo. Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia". Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili.  Ashik sasa ana meno 28. "Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware. "Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazi...

AJALI NYINGINE YA NDEGE YAUA ZAIDI YA 40

Image
Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne. ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu. Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio. Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua. Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku ...

MBASHA AKANA KUMBAKA SHEMEJI YAKE

Image
KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa. Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani. Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti. Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli. Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa ...

DIAMOND ATAJWA KUWANIA TUZO ZA TFAAS,KUCHUANA NA YAYA TOURE

Image
Diamond Platinumz anaendelea kuongeza CV katika muziki wake kwenye level za kimataifa baada ya kutajwa Jana kuwa mmoja kati ya vijana wa Afrika wanaowania tuzo kubwa ya The Future Africa Awards& Summit (TFAAS 2014) zitakazofanyika Lagos Nigeria, July 31. Waandaaji wa tuzo hizo wametangaza vipengele kumi vyenye majina matano katika kila kipengele baada ya kupokea mapendekezo kutoka katika bara zima la Afrika kupitia kamati yake maalum. Utoaji wa tuzo hizi unatajwa kuwa tukio la pili kwa ukubwa linalohusu vijana kaika bara la Afrika. Diamond anawania kipengele cha  The Future Africa Awards Prize in Entertainment akiwa na Ice Prince, Yaya Toure (Iviry Coast), Sarkodie (Ghana) na muigizaji Ivie Okujaye (Nigeria). Washindi wa tuzo hizi watapatikana kupitia jopo maalum lilotajwa na kamati ya tuzo hizo. Katja Schiller Nwator (Leadership Development and CSR Manager, The Tony Elumelu Foundation), Mahamadou Sy (Founder and Executive Director of the Inst...