CHRISTINA SHUSHO AANDIKA UJUMBEE HUU KUHUSU WIMBO WA ALIKIBA SEDUCE ME
Ni siku mbili sasa zimepita tangu mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya āSeduce Meā ambao umekuwa ukizungumziwa na watu mbalimbali wasanii na wasiokuwa wasanii na wanasiasa pia. Mmoja wa wasanii waliouzungumzia wimbo huo ni pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho ambaye anafahamika zaidi kutokana na nyimbo zake za kumsifu Mungu lakini kupitia Instagram yake aliandika huu ujumbe kwa Alikiba. āLeo unaeza kuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha seduce meā¦.eeh jamani Kiba we noma. ā Wimbo ni mzuri sana Professionally in boss ruge ās voice. ā Hauna picha za aibu , naeza watch na familia, though sijui maana ya SEDUCE ME. #team Kigoma #wamanyema oyeeeee LAST @OFFICIALALIKIBA BASI SIKU NYINGINE TUTEMBELEE KANISANI. UKIWA MFALME HUCHAGUI DINI WOTE WAKO.ā