Tuesday, 21 November 2017

ENGO LA CLOUDS MEDIA GROUP LAUNGUA MOTO

Mafundi umeme na Zimamoto wakiingia kupitia dirishani katika jengo la Clouds Media Group kuzima moto uliounguza baadhi ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
…Juhudi za kuingia ndani zikiendelea.
Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (wa pili kulia, T-shirt ya bluu) akiwa na askari, wakiangalia juhudi za kuuzima moto uliotokea.
…Akiongea na polisi.
Wafanyakazi wa Clouds na wananchi wakiwa nje ya jengo lililoshika moto.
Muonekano wa Jengo la Clouds Media Group.
 Magari ya Zimamoto yaliyofika kupambana na moto huo.
SEHEMU  ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia.
Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la Posta jijini Dar es Salaam, moto uliteketeza studio zao na kupoteza vitu mbalimbali ambapo moto wa leo umeteketeza baadhi ya ofisi za studio ya Televisheni.
Hata hivyo, alikishukuru kikosi cha Zimamoto kwa kufika haraka eneo la tukio na kuuzima moto huo.  Vilevile alisema hakuna binadamu aliyepata madhara kutokana na tukio hilo.
Mutahaba alisema juhudi zaidi zinaendelea katika kituo hicho ili kurekebisha mambo yaliyotokea na kwamba ratiba zao zitaendelea kama kawaida.CREDIT:GPL

Rais Magufuli awaonya Masha na Msando

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho leo kwenye mkutano mkuu wa NEC unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi.

Wengine ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda

Akiongea baada ya kuwapokea wanachama hao Rais Magufuli amesema, “Nawaomba msije mkabadilika tena, mmekuja huku na wanachama wamewakubali msirudi tena kule, hiki ni chama cha wote hata watoto watazaliwa watakikuta na watajiunga kwasababu kina misingi imara, kwahiyo msije huku kujaribu”.

Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalinmbali ndani ya chama na kwenye maeneo yao. “Nyie sasa mmepitishwa na mkutano mkuu wa NEC hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwapinga na kama kuna nafasi ya kugombea huko nendeni mkagombee ili mje mshiriki kuijenga nchi na Chama”..

Profesa Kitila, Katambi, Msando waingia CCM

Dar es salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando.

Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."

Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.

Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.

"Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.

Kwa upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga mkono.

"Lakini ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto, wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”

Yeye Msando amesema  baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.

Amesema anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.

"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.

Sophia Simba arudi CCM


Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.

Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.

"MwanaCCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi lakini tumekuwa tukinyamaza,  kikao hiki ndiyo kilimfukuza," amesema Rais Magufuli katika kikao hicho kinachofanyika leo Jumanne.

Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.

BREAKING : MWANAMKE AFANYIWA UKATILI NA MUMEWE WA KUTISHA KISA KUPATA KAZI,AMWAGIWA TINDIKALI

Mwanamke mmoja kutoka katika wilaya ya Malwani, Mumbai nchini India amejikuta akipata kilema cha kudumu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na mumewe siku mbili baada ya kupata ajira serikalini.Zakira Ali SheikhMwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Zakira Ali Sheikh (26) amesema alikatazwa na mumewe ‘Roobab Ali Sheikh’ kutafuta kazi yoyote ya kuajiriwa na kuambiwa kuwa abaki tu nyumbani kwa ajili ya kulea familia na kazi ndogo ndogo.

Mwanamke huyo wakati anasimulia kisa hicho kwenye mahojiano yake na gazeti la Hindu Times la nchini India amesema mumewe alikuwa ni fundi magari na alikuwa haachi pesa ya matumizi nyumbani kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kichwa jinsi ya kuendesha familia yao yenye watoto wawili.Bi. Zakira ambaye tayari jicho lake moja limeshapata upofu amesema alishindwa kuvumilia hali hiyo ndipo alipoamua kupeleka maombi ya kazi kwenye kiwanda cha Serikali cha Sabuni baada ya kuona matangazo ya kazi.
Anasema baada ya siku mbili aliona jina lake kwenye mtandao kuwa amechaguliwa kuanza kazi kwenye kiwanda hicho ndipo alifanya taratibu zote na kuanza kazi bila kumjuza mumewe.
Hata hivyo aliona sio vyema kukaa kimya ndipo siku ya tatu alipoamua kumwambia mumewe usiku na kuanza kuambulia kipigo na kisha kumwagiwa tindikali usoni.
“Nilipiga makelele usiku ule kwa muda wa dakika 10 lakini hakuna jirani aliyekuja kuniokoa hadi baadae kaka yangu alipokuja kuniokoa, niliumia sana nilijiona kama nakufa.“amesema Bi. Zakira .
Jeshi la polisi mjini Mumbai limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limesema tukio hilo limetokea tarehe 14 Novemba mwaka huu na tayari mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Kwa sasa mwanamke huyo anatibiwa katika hospitali ya Mumbai nchini humo na amewekewa mipira ya kupumulia ambapo anahitaji msaada wa Euro 29,090 sawa na Tsh milioni 76 ili aweze kukamilisha upasuaji.
Tayari mashirika binafsi yameshajitolea kumsaidia mwanamke huyo likiwemo shirika la ‘Make Love Not Scars’ kwa kumshangia dola $11,0000.

ANGALIA PICHA YA KWANZA IRENE UWOYA NA NDUGU ZAKE WALIVYO TEMBELEA KABURI LA MUME WAKEFamilia ya @ireneuwoya8 yafanikiwa kuzulu (kutembelea) kaburi la marehemu NDIKUMANA… mama mdogo na mama uwoya washindwa kujizuia… Wamwaga machozi na kugala Gala juu ya kaburi huku wakihuzunika kupita kiasi… Taarifa zilizo tufikia ni kwamba walinusurika kuzimia kutokana na Pressure iliyosababishwa na kulia sana

Monday, 20 November 2017

Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Ccm Jijini Dar Leo

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wake Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KENYA YAIDHINISHWA USHINDI WA KENYATTA


Tumefurahishwa na uamuzi wa MahakamMmoja wa waliogombea urais nchini Kenya, Ekuru Aukot, amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ambayo alisema imedhihirisha uhuru wake na kujitolea kwake kudumisha sheriaAmesema: “Wanasiasa hawawezi kuwa majaji na mahakimu.” (Majaji wa Mahakama ya Juu) Walifanya hivyo 1 Septemba walipofuta ushindi wa Kenyatta, na wamerudia tena leo,” amesema.
Tunatumai kwamba sasa Kenya inaweza kusonga mbele, na wanaochochea ghasia kutokana na mzozo wa uchaguzi sasa hakuna mzozo tena baada ya uamuzi wa mahakama. Tunaweza sasa kuangazia mambo ya uzito zaidi. Chama chetu (Thirdway Alliance) sasa kutaangazia kuhakikisha Serikali inafanya kazi ipasavyo.”

Kenyan President Uhuru Kenyatta addresses a news conference at the State House in Nairobi December 2, 2014. Kenyatta said on Tuesday he had nominated a new interior minister and accepted the resignation of the head of the police, both of whom have been criticised for failing to stop a spate of attacks blamed on Islamist militants. REUTERS/Thomas Mukoya (KENYA – Tags: POLITICS CIVIL UNREST PROFILE)ya
Duale: Wakati umefika kwa Wakenya kusonga mbele
Kiongozi wa wengi katika Bunge la Taifa, Aden Duale, amesema wakati umefika sasa kwa Wakenya kusonga mbele.
Amesema Wakenya sasa wanafaa kuangazia kuungana pamoja, na amesema kuna njia nyingi za kuendeleza umoja.
“Wakenya walipiga kura na kumchangua Kenyatta, ushindi wake ulipingwa tena na leo tuna furaha kwamba kwa kufuata sheria, ushindi wa Kenyatta sasa umeidhinishwa kwa kauli moja,” amesema.
Maraga: Majaji wameamua kesi zote hazina msingi
Jaji Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.
Kesi ya Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.
Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake..
Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21

FAMILIA YA NDIKUMANA YAZUIA IRENE UWOYA ASIPIGWE RWANDA


FAMILIA ya aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ (39), imezuia staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya ambaye alikuwa mke wa jamaa huyo asifanyiwe fujo baada ya kutinga nchini Rwanda jioni ya Ijumaa iliyopita. Hatua hiyo ilikuja baada ya Ndikumana kupoteza maisha huku Uwoya akishushiwa tuhuma za hapa na pale na kwamba huenda alichangia kifo hicho. Hamad Ndikumana ‘Katauti’ (39) enzi za uhai wake akiwa na staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichoambatana na Uwoya, familia ya Ndikumana ilichukua uamuzi huo baada ya watu mbalimbali nchini humo kuwa na hasira na Uwoya.

         Kutokana na kifo cha Ndikumana, Uwoya alilazimika kwenda Rwanda kuhani msiba akiwa na mwanaye aliyezaa na jamaa huyo, Krish, mama na baba yake na mabaunsa wa kumpa ulinzi. Chanzo hicho kilieleza kwamba, watu mbalimbali nchini humo walikuwa na hasira juu ya Uwoya kwamba ndiye aliyesababisha kifo cha Ndikumana kwani alikuwa na msongo wa mawazo akimfikiria yeye kwa kuwa alimpenda na kutaka wairudishe ndoa yao, lakini mwanamama huyo akawa anang’ang’ania apewe talaka ambayo hadi Ndikumana anafariki dunia alikuwa hajaitoa. Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya. “Mashabiki wa Ndikumana walitaka kumfanyia fujo Uwoya kwa kuwa wanadai ndiye chanzo cha kifo cha mpendwa wao, lakini familia iliwazuia wasifanye hivyo kwa kuwa walishamsamehe Uwoya ndipo hali ya amani ikawepo,” kilisema chanzo hicho.

Kiliendelea kueleza kuwa, Uwoya aliwasili nchini Rwanda Ijumaa iliyopita kwenda kuona kaburi la mumewe ambaye alizikwa Jumatano iliyopita ambapo alipokelewa vizuri na mama wa Ndikumana pamoja na familia kwa jumla. “Zile tofauti waliziweka pembeni na mama Ndikumana akamwambia wamemsamehe hivyo ikawa ni kuomboleza upya kwani Uwoya na mama’ke alikuwa akilia sana hadi kushindwa kutembea,” kilisema chanzo hicho. Hata hivyo, alisaidiwa kwa kushikwa mkono na wenyeji kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mkwewe Ndikumana kama mtoto wake.

Baada ya chanzo kutiririka, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye alikiri kupokelewa vizuri na familia pamoja na mama Ndiku ambaye alipomuona tu alimkumbatia huku akilia kwa uchungu akimuita ‘mwanangu’. Naye msanii wa filamu, Michael Sangu ‘Mike’ ambaye ni mmoja wa watu waliosafiri alikiri kuwa walipokelewa vizuri na hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza. “Uwoya, baba, mama na Krish walitangulia na ndege na walipokelewa vizuri kabisa na hakuna mtu aliyewafanyia fujo wala nini, familia imewapokea kwa ukarimu na sisi ambao tulifika baadaye maana tulisafiri kwa basi tulipokelewa vizuri sana,” alisema Mike Sangu.
CREDIT: GPL

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 20.11.2017

                                        

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI