FREEMASON WATHIBITISHA WOLPER KUWA MJUMBE WAO!!
Staa mwenye mvuto kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Wolper. BAADA ya hivi karibuni kunaswa akiingia katika jengo lao, staa mwenye mvuto kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Wolper amezidi kugandwa na skendo ya Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemason akidaiwa kuishi kwa masharti ya taasisi hiyo huku nyumba yake ikiwa imejaa vitu vinavyodaiwa kuwa vya ‘Ki-freemason’. Akizungumza na gazeti hili, ‘dada’ wa kazi wa Wolper ambaye kwa sasa ameacha kufanya kazi kwake huku akiomba hifadhi ya jina lake, alisema mbali na vitu hivyo, staa huyo anaishi kwa masharti makali kwani kila siku anaamka saa kumi alfajiri na wakati huo anamzuia dada huyo asiamke. “Akiamka (Wolper) saa kumi hiyo alikuwa akinikataza nisiamke, sikuwahi kujua huwa anafanya kitu gani akiamka na kwa nini alikuwa akinikataza, ukweli maisha yake anaishi kwa masharti ya ajabuajabu nahisi ni Freemason,” alisema dada huyo. SOMA ZAIDI