Posts

Showing posts from May 5, 2018

Mkude Atajwa Namba Sita Bora 2017/18

Image
KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote. Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara. Wakizungumza na Championi Ijumaa kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu. Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri. Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu

MAGAZETI YA LEO 5/5/2018

Image

Jinsi ya kuepuka matatizo ya nguvu za kiume

Image
MATATIZO haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla.Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano. Zipo sababu nyingi kama tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo. Mtu anaweza kuwa na tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshituko huo hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa, yaani ana tatizo. Kwa hiyo ni vema unapotokewa na tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika hospitali kubwa. AINA ZA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume. Watu wengi wamezoea ukisema tatizo la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi isivyo kawaida na ku

Huu ndiyo Ugonjwa Utokanao na Msongo wa Mawazo

Image
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi. Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi. Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo. Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo: Magonjwa ya moyo Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moy

TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA ZATIKISA JIJINI DAR

Image
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,(kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017. Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo. …Mwijage (katikati) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda . Mwijage (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zephania Shaidi kutoka Shirikisho la  Viwanda Tanzania (CTI) ambaye alipokea kwa niaba ya baadhi ya viwanda vilivyofanya vizuri ambavyo wawakilishi wake hawakuwepo. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwijage (katikati). SHIRIKISHO  la Viwanda Tanzania (CTI) leo limetoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017 ambazo zimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage. Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz