Posts

Showing posts from July 20, 2017

Mama Mzazi wa Zari, Afariki Dunia!

Image
Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ , Halima Hassan amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali. Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinums , amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram , na haya ndiyo ameyaandika;   Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga . Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka. Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga , aliyeaga dunia M

TUNDU LISSU AKAMATWA AKIWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA KWENDA RWANDA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo. Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Usalama Barabarani Yamkuta, Afutwa Kazi

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam – Arusha, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Pwani. NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana. Masauni (kushoto) akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express. “Mwaka jana nilipofanya zia

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA MKOA WA SONGWE

Image
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe, Elias Nawela baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Kat

BREAKING NEWS: SIMBA YAMSAJILI KIPA BORA WA COSAFA

Image
Saidi Mohammed. Katika kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18, Klabu ya Simba imeendelea kufanya kweli kwa kusajiri wachezaji wanaoweza kuleta ushindani katika kikosi cha kwanza. Habari ni kuwa Simba imemsajili kipa Saidi Mohammed kwa kandarasi ya miaka miwili. Said alikuwa kipa wa Mtibwa Sugar na kwa sasa yupo katika kikosi cha Taifa Stars, pia ndiye aliyekuwa Kipa Bora wa Michuano ya Cosafa iliyofanyika nchini Afrika Kusini, mwaka huu.

Waliomvua mwanamke nguo wahukumiwa kifo Kenya

Image
Wanaume watatu ambao walimvamia, wakamvua nguo na kumuibia mwanamke ndani ya basi la abiria mjini Nairobi, katika kisa ambacho kilirekodiwa na kusambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii miaka mitatu iliyopita, wamehukumiwa kifo kwenye mahakama moja mjini Nairobi. Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa baada ya watatu hao kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia nguvu. Kifungo kingine cha miaka 25 kilitolewa kwa kumvua nguo mwanamke huyo, Jilo Kadida. Kifungo cha miaka 25 hata hivyo kilitupiliwa mbali kwa wanaume hao walikuwa tayari wamehukumiwa kifo. Wanaume hao watatu ni dereva wa basi Nicholas Mwangi, na makondakta wake Meshack Mwangi na Edward Ndung'u. Hakimu wa Nairobi Francis Andayi, alisema kuwa kitendo hicho kilikuwa kibaya walichoonekana kufurahia, kwa sababu walikuwa wakishangilia huku wakimvua nguo mwanamke huyo. Muathiriwa aliiambia mahakama kuwa kulikuwa na karibu wanaume saba ndani ya basi wakati huo, ambao walitaka kumbaka lakini akadanganya kuwa a