Posts

Showing posts from September 2, 2016

UJUMBE WA VANESSA MDEE KWA JUX WA WAKUNA WENGI

Image
Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ametumia fursa ya siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, ambaye pia ni Staa wa muziki wa R&B hapa Bongo, Juma Jux kumwandikia ujumbe muhimu kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda huku akiutaja wimbo wao wa pamoja, #Wivu kuwa ndiyo nguzo ya kukutana na kuanzisha uhusiano wao: Kuoitia ukurasa wake Instagram, Vee Money ameandika; When we first met I was an upcoming songstress with a fast tongue and one hit song on the radio. You … well you were pretty much the same. Your boy asked me if I would spit some bars on your song. I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a change of heart. Fast forward to 2yrs later, tumekuwa. You’ve got the biggest song in the country #Wivu and a multi million dollar brand #AfricanBoy and as for me well … kitu kimoja hakijabadilika though. Kwako sisikii. Lol! Lakini hayo yoteee ni mifano tu ya jinsi gani ukiwa na mahusiano na mtu anayekujenga kifikra na vinginevyo ...

JPM Kubadili Noti Kuwakomoa Walioficha Mabilioni Majumbani

Image
Rais John Magufuli amewataka watu walioficha fedha majumbani kuziachia ziingie kwenye mzunguko vinginevyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa kuzipeleka.  Amesema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao katika benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho, hivyo akawataka kuachana na tabia hiyo kwa sababu fedha hizo ni mali yao. Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jana, Rais Magufuli aliyetumia dakika 73 kuzungumza na wahandisi hao na kueleza mikakati na changamoto zinazoikabili Serikali ukiwamo wizi na ufisadi, alisisitiza;   “Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na wahandisi kuto...