Posts

Showing posts from October 28, 2017

MATUKIO YA SHEREHE HARUSI YA JOTI YAZIDI KUFANA USIKU HUU UKUMBI WAMLIMANI CITY,THE COMEDY WOTE NDAN.

Image

Mbunge:Bobi Wine Amekataa Fedha Milioni 29 Alizohongwa

Image
Mwanamuziki Uganda, ambaye ni Mbunge Kyadondo East , Bobi Wine amekataa fedha milioni 29 za Uganda alizohongwa na serikali ili aweze kukubaliana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho kipengele cha katiba na kuondoa ukomo wa miaka 75 kuongoza nchi. Bobi Wine ameiamuru benki ambayo amewekewa fedha hizo kuzirudisha kwa watu ambao wameziweka na kusema kutokana na taarifa ya mawasiliano wabunge wote wa Uganda 449 wamepewa fedha hizo ili waweze kukubaliana na hoja hiyo na kuoandoa ukomo wa miaka 75 ili kuweza kumpa nafasi tena Yoweri Kaguta Museveni (73) kugombea nafasi ya Urais tena kwa awamu ya sita 2021. “Oktoba 24, 2017 Milioni 29 wa Uganda ziliwekwa kwenye Account yangu ya benki, pesa hizo walipewa wabunge wote wa Uganda kwa mujibu wa taarifa rasmi pesa hizo walizopewa wabunge ni ili kukubaliana na pendekezo la kufanyia marekebisho kipengele cha 102 (b) cha Katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa miaka 75 kama sifa ya kusimama kama Rais wa Uganda” alisema Bobi W...

ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA MOBETTO MAPYA TENA,WAONYWA VIKALI,WAWEKWA KITI MOTO

Image
Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii. Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani. “Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto. Zarinah Hassan. “Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku msanii atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama yeye hataendeleza uhusiano na mama wa mtoto. Zari ni mama wa watoto wake wawili, wamedumu muda mrefu hivyo yeye ataendelea tu kushikilia usuk...

Mambo 10 Utayaona Leo Uwanja wa Uhuru…Simba vs Yanga

Image
Kikosi cha timu ya Simba. . YANGA na Simba zinakutana leo Jumamosi kila moja ikiwa imepania kushinda mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pamoja na yote, watani wanapokutana kunakuwa na burudani nyingi sana ambazo zinatofautisha aliye uwanjani na atakayeangalia katika runinga. Kwenye Uwanja wa Uhuru, idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia ni 23,000 tofauti na 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa. Pia kumbuka mechi hii ya watani inarejea kwenye uwanja huo baada ya kipindi kirefu. Kutakuwa na mengi ambayo yatajitokeza ndani na nje ya uwanja, lakini nakupa 10 tu ambayo kwa asilimia 90 utayaona. Kikosi cha timu ya Yanga Wasio na tiketi: Watu watajitokeza wengi zaidi kuliko idadi ya wale walio na tiketi na watajazana nje ya uwanja na kusababisha kero kubwa nje ya uwanja. Bado kuna tabia ya watu kuamini kuwa wanapokwenda uwanjani kuna nafasi ya kuingia angalau kwa njia za mkato. Hivyo hawatakubali kuondoka mapema badala yake watae...

SHAHIDI AELEZA WALIVYOAHIDIWA MAMILIONI KWAJILI YA KUMUUA BILIONEA MSUYA

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeelezwa kuwa washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya waliahidiwa kulipwa Sh17 milioni kila mmoja. Hayo yamo katika maelezo ya mshtakiwa wa saba, Ally Mussa Majeshi yaliyosomwa mahakamani na shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Sajini Atway Omary baada ya kupokelewa kama kielelezo.Maelezo hayo yalisomwa baada ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, kutoa uamuzi mdogo wa kukataa pingamizi la upande wa utetezi kupinga maelezo hayo yasipokelewe kama kielelezo.Jopo la utetezi linaloundwa na mawakili Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu walikuwa wakipinga wakisema mshtakiwa aliyatoa baada ya kuteswa na polisi. Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo na kuungana na hoja za mawakili wa Serikali, shahidi huyo wa 10 akatakiwa kuyasoma maelezo hayo neno kwa neno. Akisoma maelezo hayo, shahidi huyo ambaye ndiye aliyeyaandika katika Kituo cha Polisi Kigoma Oktoba 5, 2013, alisema mshtakiwa alimw...