JIJI la Arusha na Mkoa wa Manyara, hali ya hewa ilishachafuka, wingu zito limefunika kufuatia kuuawa kwa kupigwa risasi, mfanyakazi wa Kampuni ya Tanzanite One, Onesmo William Mushi (pichani). Mtuhumiwa wa mauaji hayo ni bilionea wa madini, mkazi wa Arusha, Joseph Mwakipesile ‘Chusa’ ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki migodi, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara.NA GLOBAL PUBLISHER ONESMO ALIVYOUAWA Habari zimedai kwamba Onesmo akiwa eneo lake la kazi, mgodini chini, alipigwa risasi mbili kifuani ambazo ziliondoa uhai wake. Tukio hilo lilitokea saa 8 usiku, Julai 20, mwaka huu, chanzo kikitajwa kwamba ni mgogoro wa kugombea madini. Imedaiwa kuwa Onesmo, akiwa na wafanyakazi wenzake wa Tanzanite One ambao wamefahamika kwa jina mojamoja, Kennedy na Leonard, walikutana na wachimbaji wadogowadogo hivyo kutokea mvutano wa kimaslahi. Habari zimedai kwamba miongoni mwa wachimbaji hao wadogo, alikuwepo Chusa ambaye ndiye a...