Baada ya Sintofahamu… Zitto Kabwe ajitokeza
Kiongozi Mkuu wa ACT Zitto Kabwe amejitokeza leo kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya taarifa kutolewa jana na chama chake kuwa hawajui alipo tangu juzi Jumamosi juni 11. Akizungumza na wanahabari leo baada ya kujitokeza, Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa hatishiki na vitisho vinavyotolewa na Jeshi la Polisi nakwamba amekusudia kufanya kongamano la kujadili bajeti kesho Makao Makuu ya Chama hicho huku akiitaka jeshi la Polisi kuacha kumvizia na badala yake limkamate kwa kufuata Sheria. Hii hapa ni taarifa iliyolewa jana Jumapili na uongozi wa Chama Cha ACT wazalendo kuhusu kupotea kwa Kiongozi wao Zitto Kabwe. TAARIFA KWA UMMA Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku. Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali g...