Posts

Showing posts from October 3, 2016

RAIS JOSEPH KABILA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akiangalia kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKUL...

RAIS MAGUFULI AMTHIBITISHA AMTEUA PROF. MUSERU KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI..

Image
................................................................................. RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA CUBA, IKULU JIJINI DAR LEO Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (kulia kwake) na ujumbe wake alipokutana nae Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. Makamu wa Rais wa Cuba, yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, utamaduni, michezo, kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.  Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia walioketi) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (wa tatu kushoto walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao, mara baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016

Barua Ya Baraza Kuu La CUF Kwa Msajili Wa Vyama Vya Siasa Tanzania

Image
Katibu Mkuu wa Chama CUF – Maalim Seif Sharif Hamad. BARUA YA BARAZA KUU LA CUF KWENDA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA. CUF/HQ/KM/016/10 Date: 27/09/2016 Jaji Francis S.K. Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, DAR ES SALAAM YAH: MSIMAMO NA USHAURI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU UONGOZI WA KITAIFA WA CHAMA CHA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) Tafadhali husika na somo hapo juu pamoja na barua yako ya tarehe 23 Septemba 2016 yenye Kumb Na. HA.322/362/14/85 kuhusu somo tajwa. Baraza Kuu la Uongozi la The Civic United Front (CUF) – Chama Cha Wananchi, kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama, limepokea barua yako tajwa hapo juu pamoja na taarifa fupi inayoainisha msimamo na ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa Chama cha The Civic United Front (CUF) na kuijadili kwa kina. Yafuatayo ni majibu na msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF ambayo tunapenda kuyawasilisha ili ofisi yako iyafanyie kazi. Awali ya yote, tunakupongeza kwa namna ulivyofuatilia kwa kina, ...

Diamond Akiri Mimba Ya Mobeto Kuharibika

Image
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’. BAADA ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu ujauzito alionao mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika. Mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto. Diamond aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka hayo kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya Clouds mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika. “Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho. Hamisa Mobeto akiwa katika pozi. Mimi si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa sijui kama ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea a...