MHE. BALOZI SEFUE AENDELEA KUWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUVAA BEJI ZINAZOWATAMBULISHA MAJINA YAO WANAPOKUWA KATIKA MAENEO YA KAZI
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank . Na Anna Nkinda – Maelezo Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi. Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao. ...