Posts

Showing posts from March 16, 2015

DIAMOND NUSURA AKATWE MGUU! KWA UGONJWA WA KISAHANI

Image
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata wapi aliyewahi kuwa mchumba wa Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenusurika kukatwa mguu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia ugonjwa wa Foot Corn (maarufu kwa jina la kisahani) kumtesa kwa kipindi kirefu. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond ambaye kwa sasa anaminya kimalavidavi na mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’, alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo takribani siku 730 zilizopita (miaka miwili), huku mwenyewe akipuuzia matibabu yake na kuelekeza nguvu kwenye shoo za ndani na nje ya nchi. “Mara kwa mara alikuwa akilalamikia maumivu makali ya mguu lakini kwa kuwa yalikuwa yakija na kupotea, alikuwa akipuuzia kwenda hospitali mpaka juzi (Ijumaa) alipoamua kwenda TMJ,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa jina. WALICHOKIBAINI MADAKTARI “Madaktari walipompim...