BREAKING NEWS : MSANII TUNDA MAN APATA AJALI MBAYA IRINGA
Taswira za ajali aliyoipata Tundaman leo. Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakua umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali akiwa Mkoani iringa Asubuhi ya April 17 Tunda Man. Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘ Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki ‘ Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘ Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Ki...