ANGALIA PICHA DAKTARI APIGANA NA MGONJWA WODINI MORO
Mwili wa marehemu Yasin Jailan (15) aliyekata roho ndani ya wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro huku dokta akizichapa kavukavu. Akiwa mitaani akisaka matukio, mwanahabari wetu alivutiwa waya na chanzo chetu kisha akatonywa kuwa kuna bonge la timbwili kwenye wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Timbwili! Katika hali ya kusikitisha mgonjwa Yasin Jailan (15) aliyekuwa wodini anadaiwa kukata roho huku dokta akizichapa kavukavu na wagonjwa, Ijumaa Wikienda limenasa kisa cha ajabu Morogoro ambapo alitii wito na kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri (huwa Global hatulazi damu kufika eneo la tukio). Alipofika wodini hapo, mwandishi wetu alishuhudia mtoto akikata roho huku baba mwenye mgonjwa aliyetajwa kwa jina la Jailan Mrisho akizichapa na daktari ambaye jina halikupatikana. Baba wa marehemu (kushoto) akilia kwa uchungu. Kwa mujibu wa baba mwenye mgonjwa, alimfikisha mwanaye hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria uliok...