Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu. Anadaiwa kutafuta shetani mwingine wa ugomvi baada ya ‘kumalizana’ na Aunt Ezekiel Grayson na kuanzisha ushosti na mwigizaji, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, jambo ambalo linawapa wasiwasi mashabiki wao kutokana na dhana iliyojengeka kuwa mrembo huyo (Wema), hawezi kudumu na rafiki kwa kipindi kirefu. URAFIKI WAANZIA KWENYE KAMPENI ZA CCM Mastaa hao walianza kuwa na ukaribu mkubwa kwenye mambo ya Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizozinduliwa Jumapili iliyopita katika Viwanja vya Jangwani, Dar. Habari zilieleza kwamba, kabla ya hapo, wawili hao hawakuwahi kuwa na urafiki hata zaidi ya salamu. WEMA AMPOZA BATULI Chanzo ambacho ni mtu wa karibu na wawili hao kilieleza kwamba, baada ya Batuli kupata mkasa wa kuunguliwa nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya …Mbezi Beach, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa hao walikuwa wote saluni na walipopata taarifa ya mkasa huo, Wema ndiye aliyempooza machungu Batuli kwa kumsaidia katika kipindi...