BREAKING: Polisi watoa taarifa Kuhusu tukio la mlipuko ofisi za mawakili
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 28/08/2017 TUKIO LA MLIPUKO KWENYE OFISI ZA MAWAKILI WA IMMA Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 26/8/2017 lilitoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam. Hivyo Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui. Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baa...