Posts

Showing posts from March 9, 2018

Man United Vs Liverpool, Salah Aundiwa Tume Manchester Utd

Image
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah (kulia) Paul Labile Pogba. MANCHESTER United inatarajiwa kuwa mwe­nyeji wa Liverpool, ke­sho Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford, mchezo huo ni mkubwa na unasubiri­wa kwa hamu. Kuelekea mtanange huo, gumzo kubwa ni juu ya uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah ambapo mashabiki wa Unit­ed wameanza kupata hofu kuhusu mchezaji ambaye atamzuia. Kawaida Salah amekuwa akipangwa kushambulia akitokea kulia, kwa aina ya ulinzi wa United beki wa kushoto am­baye atatakiwa kukutana naye ni Ashley Young au Luke Shaw, sasa hapo ndipo patamu, imeibuka hoja juu ya nani mwe­nye uwezo kati yao anayeweza kumficha Salah. Mchezo uliopita timu hizo zilipoku­tanaa ulimalizika kwa suluhu, huku Mar­teo Darmian akipangwa kucheza beki wa kushoto, kwa sasa beki huyo siyo chaguo la kwanza la Kocha Jose Mour­inho. Kutokana na ubora wa Salah kufun­ga, mashabiki wa United kutoka mataifa mbalimbali wamepaza sauti wa

Rais Kenyatta, Odinga Waahidi Kuwaunganisha Wakenya

Image
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga. RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo, Raila Odinga, katika ofisi yake ya Jumba la Harambee, Nairobi,a mba po viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana kuunda taifa lenye umoja. “Tumekubaliana tutawaleta pamoja wananchi na kujadiliana kuhusu matatizo yanayoathiri taifa letu na wananchi, na kuunda taifa lenye umoja na lililo imara ambapo hakuna raia anayehisi ametengwa,” alisema Rais Kenyatta baada ya mkutano huo. “Tumekutana na ndugu yangu Kenyatta, tumeongea kwa kirefu na kukubaliana kwamba tunataka kuiunganisha Kenya iwe taifa moja. Mgawanyiko ambao umekuwepo tangu uhuru utakwisha  na sisi tutembee pamoja,” alisema Raila Odinga katika hafla hiyo.

AJALI MBEYA: Wanne Wafariki Dunia, 20 Wajeruhiwa Vibaya

Image
MBEYA: Watu wanne wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas kugongana na lori jana Machi 8, 2018 katika eneo la Igawa wilayani ya Mbarali mkoani Mbeya. Ajali hiyo imetokea katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 170 DKS lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe kugongana na lori lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lililokuwa limebeba kontena. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,  chanzo cha ajali ni dereva wa basi aliyekuwa akijaribu kulikwepa tawi la mti lililokuwa limeegeshwa barabarani kama ishara ya kuonyesha kuwepo kwa gari bovu mbele yake.

Rais Magufuli awaonya wanaotaka kufanya maandamano

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John  Magufuli amevionya vyama vya siasa na wananchi ambao wamepanga kufanya maandamo siku za hivi karibuni kwa mujibu wa taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni. Amesema hayo leo, Machi 9, 2018 wakati akizindua Tawi la CRDB-Bank, Chato mkoani Geita na kuwataka waliojiandaa kutekeleza mpango waache mara mora vinginevyo watashughulikiwa. “Nchi hii ni ya amani, ndiyo maana uvunjifu wa amani ulipoanza kutokea kule Kibiti tuliamua kuufuta mara moja. Kuna watu wanadhani tunafanya siasa kila wakati, kama wametumwa na baba zao kuandamana, watawasimulia vizuri.  “Wapo Watanzania wachache ambao hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kuambiwa maneno matamu. Mimi niliomba kura kwa wananchi wangu kwa kusema ukweli, nitaendelea kusisitiza ukweli daima,” alisema Magufuli. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei ameeleza kwamba uanzishwaji wa Tawi la Benki hiyo Chato ni kutokana na utafiti uliofan