Posts

Showing posts from October 26, 2017

Matukio yaliyojiri ikiwa ni pamoja na babu abebwa mgongoni kwenda kupiga kura kenya

Image
Leo tarehe 26 Oktoba, 2017 Taifa la Kenya limefanya uchaguzi wa Rais, ambapo kiongozi wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga amesusia uchaguzi huo. Rais Uhuru Kenyatta akipiga kura mapema leo jijini Nairobi katika Shule ya Msingi Mutomo Hadi sasa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa mtu mmoja amshauawa kwenye vurugu zilizotokea mjini Kisumu na wengine 20 wakijeruhiwa kwenye vurugu zilizoongozwa na wafuasi wa vyama vya upinzani. Misururu mirefu ya wapiga kura, katika shule ya msingi ya Kayole One, Embakasi Central jijini Nairobi Wafuasi wa upinzani wakiweka magogo katikati ya barabara mjini Migori Jaji Mkuu nchini Kenya, George Maraga akipiga kura mapema leo katika shule ya msingi ya Bosose, Nyamira Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Munaini, Othaya. Mpiga kura akiwa na Babu yake mgongoni akimpeleka kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Kaare Kaunti ya Thar

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA NAFASI MBALIMBALI ZA WAKUU WA MIKOA,MABALOZI NA MAKATIBU WAKUU

Image
Rais Magufuli Uteuzi wa Rais Magufuli, uliotangazwa leo Alhamisi Oktoba 26,2017 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi uliwahusu pia, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na wakuu wa mikoa ambao wataapishwa kesho Ijumaa Oktoba 27,2017 mchana Ikulu jijini Dar es Salaam. Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Mkoa wa Manyara – Mkuu wa Mkoa ni Alexandar Pastor Mnyeti (Alikuwa DC wa Arumeru) Mkoa wa Rukwa – Mkuu wa Mkoa ni Joachim Leonard Wangabo (alikuwa DC wa Nanyumbu) Mkoa wa Geita – Mkuu wa Mkoa ni Bwana Robert Gabriel Lughumbi (alikuwa DC wa Korogwe) Mkoa wa Mara – Mkuu wa Mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima (aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne) Mkoa wa Dodoma – Mkuu wa mkoa ni Bi. Christine Solomoni Mndeme (alikuwa DC wa Dodoma Mjini) Mkuu wa Mtwara – Gelasius Gasper Byakanwa (alikuwa DC wa Hai) Uteuzi wa Mabalozi Dr. Aziz P. Mlima – Amekuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu wizara mambo ya nje) IGP Mtaafu Ernest Mangu – Amekuwa Balozi Hawa Vituo vyao vya k

Kangi Lugola: Kwa Nini Kasri la Mama Rwakatare Halijabomolewa?

Image
NAIBU Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kufikisha mezani kwake maelezo ni kwa nini nyumba ‘kasri’ ya mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) haijabomolewa. Lugola ametoa muda kwa Nemc hadi kesho Alhamisi Oktoba 26,2017 saa 10:00 jioni awe amepata taarifa ya maandishi ili aweze kutoa uamuzi iwapo ibomolewe au la. Naibu waziri ametoa agizo hilo leo Jumatano Oktoba 25,2017 wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipokutana na watendaji wa Nemc. Lugola amefikia uamuzi huo baada ya Nemc katika taarifa yake kueleza serikali imeshindwa kuivunja nyumba hiyo kutokana na zuio lililopelekwa mahakamani na Mchungaji Rwakatare tangu mwaka 2012. Nemc imesema kesi ikiisha na uamuzi kutolewa hakutakuwa na shaka wala kigugumizi katika kuivunja nyumba hiyo. Kwa kauli hiyo, Naibu Waziri Lugola amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba,

BREAKING NEWS:Mwenyekiti wa IEBC Aahirisha Uchaguzi Kenya

Image
Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati. Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati aahirisha uchaguzi kwa baadhi ya maeneo nchini Kenya mpaka siku ya Jumamosi Oktoba 28, 2017 kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto mbalimbali kama vile mvua kubwa. Wafula Chebukati ametaja maeneo ambayo uchaguzi umeiarishwa kuwa ni pamoja na Kisumu Migori, Siaya na Homabay na kuwa katika maeneo hayo uchaguzi utafanyika siku ya Jumamosi, Oktoba 28. Chebukati amesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na maeneo hayo kuwa na changamoto mbalimbali ikiwepo masuala ya usalama pamoja na mvua jambo ambalo limefanya zoezi la kupiga kura kuwa changamoto ka wapigaji kura.

Mama Aolewa Na Mwanaye Baada Ya Kumpa Ujauzito

Image
Betty Mbereko na mwanaye, Farai Mbereko. BETTY MBEREKO (40) mwanamke anayeishi Mwenezi huko Masvingo, Zimbabwe, ameolewa na mwanaye wa kumzaa aitwaye Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23. Katika hali hiyo ambayo ilitokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, mama huyo anategemea kupata mwanaye ambaye pia ni mjukuu wake.  Mwanamke huyo amekuwa mjane kwa miaka 12 iliyopita ambapo amekuwa akiishi na mwanaye huyo. Alithibitisha hivi karibuni kuwa ana ujauzito wa miezi sita na hivyo akaona afadhali “aolewe” na mwanaye kwani hakutaka kuolewa na mmoja wa wadogo wa marehemu mumewe, aliosema wanamtamani. Betty aliishangaza mahakama ya kijijini kwake aliposema alianza kuzini na mwanaye miaka mitatu iliyopita.  Alisema baada ya kutumia fedha nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha mumewe, aliona ana haki ya kufaidi fedha ya mwanaye na si mwanamke mwingine. “Tazama, nilihangaika kumsomesha mwanangu na hakuna aliyenisaidia.  Sasa mwanangu anafanya kazi na watu wanas

MVUA ZASABABISHA HUDUMA ZA USAFIRI BARABARA YA MOROGORO KUFUNGWA

Image
Mvua ya inayoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Dar es salaam, imesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji hayo yamefunga mawasiliano ya barabara ya Morogoro, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi mjini. Mpaka sasa umeripotiwa kuokotwa katika mto kenge uliopo Tabata jijini humo, mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume. Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka. Kituo cha mabasi ya mwendo kasi cha Fire kikiwa kimesimama kutoa huduma kwa abiria baada kujaa maji kwa bonde la Jangwani na kufunika barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2017. Mbunge wa Jimbo la Ilala Iddi Azan Zungu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika eneo la Jangwani lilolokumbwa na mafuriko na kusababisha barabara ya Morogoro kufungwa kufuat

Wazee wa Baraza: Lulu Alimuua Kanumba Bila Kukusudia

Image
Lulu mwenye (kilemba chekundu) akiwa amejiinamia, kulia ni mama yake na kushoto baba yake wakisubiri kesi kuanza. Mama Lulu (kulia) akisubiri kwa umakini kesi ianze. Ndugu wa Kanumba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa mahakamani hapo. Lulu akiondoka mahakamani huku amejifunika kanga baada ya kesi yake kuahirishwa. …Akitolewa nje. Mama Lulu akiingia kwenye gari ili kuondoka. Mzee Michael Kimemeta akijiandaa kuingia kwenye gari. IKIWA ni wiki moja sasa tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ianze kusikiliza mfululizo kesi inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ , wazee wa Baraza la mahakama hiyo leo Oktoba 26, 2017 wametoa maoni yake kuwa Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Katika maoni hayo yaliyotolewa na Jopo la Wazee watatu wa mahakama kwa nyakati fofauti, wote wamesema Lulu alimuua msanii mwenzake huyo bila kukusudia. Awali k abla ya kutoa maoni yao, Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Sam Rum