Posts

Showing posts from September 23, 2013

ALIYEMJERUHI AUNT EZEKIEL KWA CHUPA APANDISHWA KIZIMBANI...!!

Image
Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo. Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya. Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo. Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi. Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena. Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

NATAKA KUPATA MTOTO MWINGINE HARAKA ILI BAADA YA HAPO NIJIKITE ZAIDI KATIKA FILAMU - DAVINA

Image
Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Halima Yahaya(Davina) amesema kuwa anataka kupata mtoto mwingine haraka kabla ya aliyemzaa miezi ya karibuni hajawa mkubwa  ili amalizane na kazi ya ulezi na ajikite zaidi katika kazi zake za filamu. "unajua nimeona kuwa kulea siyo kitu cha muda mchache hivyo unatakiwa umalize kwanza ndiyo uendelee na kazi zako ambapo nimeona ni bora nitafute mwingine haraka haraka ndipo nijikite katika filamu" alisema Davina akizungumza na Globalpublishers. Davina ameigiza filamu nyingi na hivi karibuni filamu yake mpya ya Sababu Ya Nasra akiwa na Slim Omar iliingia sokoni na kwasasa yupo location akishuti filamu mpya na King Majuto, Jenifer Kyaka(Odama) na Rachel Haule.  Davina

LOVENESS LOVE ADODOSHA CHOZI BAADA YA KUPIGWA KIBUTI NA PREZZO

Image
Kwa mara ya kwanza, Diva ameamua kufunguka kuhusu KIBUTI alichopewa na jamaa yake wa Kenya maarufu kwa Jina la Prezzo ambaye alikuwa amemwanika mitandaoni... Bahati  Mbaya  hali  ya  mambo  haikuwa  nzuri...Prezzo  alifanya yake  na  kisha kumtenda  dada  wa  watu.... Akiwa  bado angali  na  machozi  ya  ROHONI, Diva  ameamua  kutoa  onyo  kali  kwa  mashabiki  wake  na  kuwataka   kutolitaja  tena  jina  la  Prezzo  kwa  kuwa  hahitaji  hata  kulisikia. HUU  NI  UJUMBE  WAKE: "Hey Guys Pliz Kwa Heshima Zote na taadhima naomba msiwe mna comment about Huddah Or Prezzo in My Page. That Chapter is closed muda mrefu sana and matter of fact Dont need Drama. My Life seems to be Naturally . I never have plans for where it’s going to take me. Huwa na...

HIVI NDIVYO JANA USIKU FIESTA ILIVYOFANA SHINYANGA

Image
 Anajiita Mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake kwa shangwe huku mayowe yakitawala kila kona ya uwanja wa Kambarage usiku huu ndani wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea kurindima usiku huu.  Mtoto wa Mama Said a.k.a Chege akiimba kwa hisia jukwaani. Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake.  Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoko akiimba jukwaani usiku huu sambamba na madensa wake (hawapo pichani).  Tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu. Mashabiki wake wanamuita Kinga Zilla kutoka Sala Sala,lakini pia jina la Godzilla limemuongeza umaarufu kwa mashabiki wake kutokana na umahiri wake wa kushusha mistari ya hip hop mikavu mikavu,kama aonekavyo jukwaani akiwaimbisha mashabiki wake ndani ya uwanja wa Kambarage usiku huu.   Baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa ...

HUYU NDIYE MSANII WA KIKE ALIYEFANYA UFUSKA KWA MIAKA MINGI

Image
SIKU chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfu mo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya. Akiongea  na  mwandishi  wa  habari  hii, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.   “Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa. Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani. Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la...

MWANAMKE ANASWA NA KILO 7 ZA BANGI KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIA ALIPOKUWA AKIELEKEA NCHINI UTURUKI.

Image
MWANAMKE mkazi wa jijini Arusha, Farida Ismail (29) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na kilo 7 za bangi. Inadaiwa mtuhumiwa alikuwa ameficha bangi hiyo kwenye begi lake kwa kushona mfuko wa ndani. Alikamatwa jana saa 10.20 alfajiri baada ya mzigo wake kufanyiwa upekuzi na maofisa wa uwanja wa ndege. Alitaka kusafiri kwa ndege TK673 aina ya Boeing 738 iliyokuwa ikienda Istanbul, Uturuki. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alikiri kuwepo kwa tukio hilo . "Ni kweli tukio hilo lipo na limetokea muda huo huo uliosema yaani alfajiri, lakini sasa hivi nipo nyumbani lakini kesho (leo) nitatoa taarifa kamili,’’ alisema Kamanda. Kwa mujibu wa taarifa kutoka uwanjani hapo, maofisa wa ukaguzi wa KADCO walipopekua, awali hawakugundua kama kuna bangi katika begi la mama huyo hadi hapo walipojiridhisha kwa mara ya pili ndipo waligundua ilipokuwa imeshonewa kwenye begi. ...

"BREAKING NEWZ"MATUKIO YA HIVI PUNDE KUTOKA WESTGATE NAIROBI KENYA

Image
Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate...     14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa 14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa 14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili 14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi walioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao Moshi mkubwa ukitoka n...

UPDATE: OPERESHENI YA KUWAKOMBOA MATEKA WANAOSHIKILIWA NA AL-SHABAAB HUKO NAIROBI KUKAMILIKA MUDA MCHACHE KUANZIA SASA

Image
Jeshi la Kenya limefanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate na wanaendelea vema na operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na kuteka eneo hilo jumamosi mchana. Msemaji wa jeshi la kenya kanali Cyrus Oguna amethibitisha operesheni ya kuwakomboa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Alshabab imefikia hatua ya mwisho na inaweza kutamatika muda wowote. Idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka na kufikia 69 wakati majeruhi wakifikia 175 kwa mujibu wa serikali nchini Kenya.Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine wamefanyiwa upasuaji. Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha hofu miongoni mwa mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa makuu...

OMMY DIMPOZ AFANYA SHOW KALI MARYLAND UNITED STATES OF AMERICA

Image
 Ommy Dimpiz akiwajibika stagen licha ya mvua kunyesha lakini watu awakukosa kusemana nujuu ya  Wapenzi wa Dimpos wakipagawa na tupogo njimbo mpya ya Dimpoz  Shabiki wa Dimpos akiwa amesha jikabizisha kwenye stage akisho love kwa Dimpoz  Ukodak wa vijimambo wapenzi wa Dimpos  DMK ndiyo aliefanisha safari ya Dimpos ni mtu lol  Mambo ya Tupogo yaliyo jili ndani ya Maryland, Kwa picha zaidi nenda