Posts

Showing posts from March 28, 2018

Mahakama Yaamuru mmiliki wa IPTL Akatibiwe Muhimbili

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder  Sethi akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo kulalamika afya yake imearibika sana. Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni 309. Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo March 28, 2018 kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi. Baada ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; 'Afya yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.' Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu. “Naamuru mshtakiwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili afya yake iwe njema,” amesema

BASATA Yakanusha Kuzifungulia Nyimbo Mbili za Diamond

Image
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema nyimbo mbili za Diamond, hazijafunguliwa kama inavyodhaniwa. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema nyimbo za Wakawaka na Hallelujah hazijafunguliwa na jambo hilo halina ukweli wowote na kuwataka wananchi kulipuuza. Kadhalika, Mngereza ametoa ufafanuzi kwa nini msanii Diamond amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza na sio wasanii wengine. Mngereza ametoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa taarifa iliyoeleza msanii huyo kakutana na mawaziri hao. Baada ya taarifa hizo, kulizuka gumzo mitandaoni ambapo watu walihoji kwa nini wakutane na msanii huyo wakati kuna waliofungiwa nyimbo zao kama yeye na wengine kufungiwa kufanya muziki kwa miezi sita. Mngereza amesema hatua hiyo imetokana na majibizano yaliyokuwa yanaendelea kati ya Diamond na naibu waziri Shonza na ndio sababu iliyowafan

Vyakula vya Kukufanya Usizeeke

Image
KIINI CHA YAI L EO kwenye safu hii nitakuletea vyakula ambavyo ukila vitakufanya usizeeke kwani siku hizi watu wanazeeka haraka licha ya kuwa na umri mdogo.  Kama unataka kusafisha ubongo wako ambao huchoka mara kwa mara tumia kiini cha yai, kina wingi wa Klorine ambayo ni virutubisho muhimu vinavyowezesha ubongo kufanya kazi. COCOA Kama unafanya urembo wa ngozi hasa chini ya macho kwenye ngozi inayoweka weusi paka cocoa ina wingi wa vitamin itakayosaidia kulinda ngozi yako isizeeke. KAHAWA NA MAFUTA YA NAZI Kama unataka kuwa na nguvu kwa siku chukua kahawa yako iweke na vijiko viwili vya chai vya mafuta ya nazi kisha kunywa. Mafuta ya maboga kwa kuondoa msongo wa mawazo, Kama wewe ni mtu mwenye msongo wa mawazo mara kwa mara tumia mafuta ya maboga yana wingi wa asidi ya amino na glutamate ambayo yanasaidia ubongo kukaa sawa na wewe kujisikia vizuri. Mafuta haya ni mazuri kuyatumia hata kwa mtu mwenye mba kichwani ili kuzitibu yapake kwenye ngoz

JK' kuwa mgeni rasmi katika harambee

Image
RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kukusanya fedha kiasi cha Sh. bilioni moja, kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Lindi iliyoungua Julai 2016. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema harambee hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam. Zambi alisema maandalizi yote kwa ajili ya harambee hiyo yamekamilika na inatarajia kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya elimu nchini. Alisema harambee hiyo imepanga kukusanya Sh. bilioni moja ikiwa ni karibu nusu ya mahitaji ya Sh. bilioni mbili zinazotakiwa kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe. “Kutokana na fedha tutakazokusanya, tumepanga ujenzi uanze wakati wowote. Zoezi hili litakwenda sambamba na mpango wa mkoa kuboresha mfumo mzima wa masuala ya elimu toka ngazi ya awali,” alisema Zambi. Mkuu wa mkoa huyo alikiri kuwa mkoa wake ni mmoja kati ya inayofanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa,

Rungwe aliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu zake

Image
Mwanyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe ameliomba jeshi la polisi kusaidia upatikanaji wa Mpwa wake Saida Hilal (40) na mumewe Abdallah Kutiku ambao hawajaonekana tangu Machi 26, 2018 majira ya asubuhi. Hashim Rungwe amesema hayo leo Machi 27, 2018 na kudai Saida Hilal aliaga wenzake ofisini na kwenda kituo cha polisi kufuatilia suala la mume wake Abdallah Kutiku ambaye alichukuliwa na polisi "Huyu binti alikuwa anafuatilia habari za mumewe polisi kwa kuwa mumewe alikuwa amekamatwa na polisi hivyo naye hapatikani kwa hiyo wote wawili hawaonekani kwani tulipofika kituo cha polisi walisema hawa watu hatuwafahamu na wala hawajafika pale, tangu hapo Bi. Saida Hilal hapatikani kwenye simu zake na tumefanya jitihada kumtafuta kwenye vituo vya polisi na mahospitali kama Muhimbili, Mwananyamala na sehemu zingine za usalama bila mafanikio" Rungwe aliendelea kuelezea kuwa "sehemu zote ambazo alikuwa anapenda kutembelea zote tumepita na

Linex azungumzia ishu ya kupotezwa na Ulevi

Image
Sunday Mangu ‘Linex’ MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufungukia tetesi zinazozagaa dhidi yake kuwa ulevi ndiyo umempoteza kimuziki na kusema siyo kweli bali wanaozungumza hivyo ni wabaya wake ambao hawana nia nzuri kwake. Akipiga stori na Risasi Vibes, Linex alisema kuwa muziki ni kama biashara nyingine na mtu anaweza kushuka na kupanda hivyo kilichompoteza ni changamoto za maisha kuwa nyingi na kushindwa kuzimudu ila anaamini atarejea tena na kuwa kama alivyokuwa zamani. “Wanaosema kwamba nimepotea kimuziki kisa ulevi hawana nia njema na mimi, mwanamuziki yeyote anaweza kupotea bila kujali umaarufu alionao, ndiyo maana hata Bill Gates leo anaweza kuwa namba moja kwenye listi ya matajiri duniani na baada ya muda hata kwenye kumi bora akawa hayumo tena,” alisema Linex. Linex azungumzia ishu ya kupotezwa na Ulevi Muungwana Blog 5 Wednesday, March 28, 2018 Sunday Mangu ‘Linex’ MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufu

MAKONDA: UKIMPA UJAUZITO MWANAMKE DAR UJIPANGE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wataalamu hao. . …Makonda akiendelea kuzungumza katika tukio hilo. Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kisheria waliohudhuria kwenye hafla hiyo. Mkutano huo na wataalamu wa kisheria ukiendelea. JOPO la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maofisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria linalotaraji kuanza Aprili 9 mwaka huu. Akizungumza na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na baba zao. Makonda amesema lengo la zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumw