Fainali Uefa Champions League… Leo Shughuli Ipo
NA MWANDISHI WETU SIYO siri leo Jumamosi watu duniani watasimamisha shughuli zao kwa muda kutazama fainali ya 62 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayozikutanisha Juventus na Real Madrid kwenye Uwanja wa Millennium. Mwamuzi Felix Brych wa Ujerumani ndiye atakayechezesha mechi hii kali iliyojaa historia nyingi ambayo ni ngumu kutabiri mshindi moja kwa moja. Mpaka inafi ka fainali chini ya Kocha Massimiliano Allegri, Juventus iliitoa Monaco kwa jumla ya mabao 4-1, wakishinda mabao 2-0 halafu 2-1. Madrid ikiongozwa na Kocha Zinedine Zidane iliitoa Atletico Madrid kwa jumla ya mabao 4-2. Madrid ilishinda 3-0 halafu ikafungwa 2-1. Fainali hii inakumbusha fainali ya Uefa ya Mei 20, 1998 ambapo timu hizi zilikutana kwenye Uwanja wa Amsterdam na Madrid ikashinda bao 1-0 lililofungwa na Predrag Mijatovic. Ni miaka 19 sasa tangu timu hizo zilipokutana katika fainali hiyo, wakati huo Zidane alikuwa akiichezea Juventus sambamba na Kocha wa Chelsea sasa, Antonio Conte....