TEF WAFUNGULIA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAULMAKONDA.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) wakiondoa zuio la kutokutoa habari yoyote kwenye chanzo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye vyombo vya habari sasa kuanzia leo habari za mkuu wa Mkoa wa Mkoa zitakuwa zikitoka kwenye vyombo vya habari. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Jukwaa la wahariri kuondoa zuio kutotoa habari zamkuu wa ,Mkoa wa Dar Es Salaam leo. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ...