Posts

Showing posts from July 23, 2017

FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!

Image
Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili. Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa.  Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya m

RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO

Image
Mh.David Kafulila Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana. Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa. "Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulil

Samatta Aandika Historia Mbele ya Rooney, Aifunga Everton

Image
KRC Genk vs Everton. Mtanzania Mbwana Samatta ameandika historia ya kuwa Mtanzania aliyeweza kufunga bao dhidi ya timu ya Everton ambayo inashiriki Ligi Kuu ya England baada ya kufanya hivyo katika mchezo wa kirafiki akiwa ndani ya jezi ya KRC Genk. Samatta ambaye amekabidhiwa jezi namba tisa hivi karibuni katika kikosi hicho, amefanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao katika dakika ya 55 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton ambao walikuwa na staa wao, Wayne Rooney. Bao la Samatta lilipatikana baada ya kupigwa pasi zaidi ya saba kuanzia kwa kipa wa Genk hadi mpira ulipomfikia Samatta ambaye alimalizia kwa kupiga shuti kali. Mchezo huo uliochezwa Jumamosi hii nchini Ubelgiji ni maalum kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa 2017/18 kwa timu zote mbili. Bao la Everton lilifungwa na Rooney katika dakika ya 45. Samatta amekuwa na mwendelezo mzuri katika mechi za maandalizi ambapo wiki iliyopita pia alifunga bao moja katika sare ya maba