Posts

Showing posts from February 29, 2016

Flora Mvungi: Sijawahi kutumia ‘Uzazi wa mpango’, ‘Nazaa’ haraka haraka ili niwe huru na Uigizaji baadae

Image
Staa wa Filamu Flora mvungi ambaye pia ni mke wa mwanamuziki H.Baba, amejibu shutuma zinazoongelewa na watu kuwa anazaa haraka haraka mno ambayo ni hatari kwa afya yake. Kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Flora amesema kila mtu ana maamuzi yake kwa kile ambacho anakifanya na yeye ameamua kuzaa haraka haraka ili akirudi kwenye uigizaji awe huru zaidi na kazi yake. “Nataka nifikishe watoto wanne, kwa hiyo sasa hivi naenda kupata watatu, nahitaji nikianza kuigiza niwe free zaidi sitakuwa na majukumu ya uzazi tena” Akijibu swali kama amewahi kutumia au kuzingatia uzazi wa mpango, Flora amedai tangu aanze kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi mpaka leo hajawahi kujaribu wala kutumia uzazi wa Mpango. H.Baba na Flora wamejaaliwa kupata watoto wawili, Tanzanite na Africa huku wakitegemea kupata mtoto wa tatu hivi karibuni

Mbowe Apinga Watumishi wa Umma Kutumbuliwa MAJIPU Bila Kupewa Nafasi ya Kusikilizwa Kwanza

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amepingana  na  sera  ya  Rais John Magufuli  ya kuwatumbua majipu watumishi wa umma wazembe na wabadhilifu wa mali za umma. Mbowe amedai kuwa Serikali Magufuli imekuwa ikiwatimua watumishi mbalimbali wa umma bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kupitia kampeni ya kupambana na ufisadi, inayotambulishwa kwa kaulimbiu ya ‘utumbuaji majipu’. Akizungumza jana katika ibada maalumu ya shukrani kwa kumaliza uchaguzi mkuu salama, iliyofanyika kwenye Usharika wa Nshara wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT na kuhudhuriwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Frederick Shoo, na maaskofu wastaafu Dk. Erasto Kweka na Dk. Martin Shao, Mbowe alisema (wapinzani) hawaridhishwi na hatua ya serikali ya Rais Magufuli kuendeleza timuatimua na kuwasimamisha kazi watumishi wa umma 160 tangu aingie madarakani bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani...

IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA

Image
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015. Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News. Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa...

Kinara wa Uporaji Access Bank Mbagala Atiwa Mbaroni...Mawasiliano ya Simu yasaidia Kumnasa

Image
Siku nne baada ya majambazi 12 kuvamia Benki ya Access tawi la Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuiba Sh. milioni 20 na kusababisha vifo vya watu sita, mtu anayedaiwa kuwa kinara wa uhalifu huo ametiwa mbaroni baada ya kutajwa na washirika wake, akiwamo aliyekamatwa  akiwa anafunga ndoa. Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili ilizipata zinaeleza kuwa, kinara wa ujambazi huo alikamatiwa Sinza Mori, wilaya ya Kinondoni jana, saa 11:00 jioni. Kwa mujibu wa taarifa ambazo Nipashe ilizipata, kikosi kinachoshirikisha askari wa majeshi mbalimbali ikiwamo, polisi na la wananchi wa Tanzania, kilinasa watu wanne kwenye sherehe ya harusi baada ya kufuatilia mawasiliano yao ya simu.  “Unajua sasa hivi hili suala linahusisha jeshi ambao wamefuatilia kwenye mtandao na kunasa simu za watu wanne ambao wamekamatwa huko Mbagala, akiwamo bwana harusi na watu wengine wanne,” kilisema chanzo chetu. Taarifa hizo zinasema baada ya watu hao kukamatiwa wakiwa wanafunga ndoa ms...