Posts

Showing posts from August 25, 2016

Mbatia: Rais Apeleke Muswada Bungeni Kufuta Vyama vya Siasa

Image
    Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Mbatia (wa pili kushoto) akionesha hisia zake mbele ya wanahabari. Mkutano ukiendelea. Wanahabari wakichukua tukio hilo leo Agosti 25, 2016. Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari. NA DENIS MTIMA MWENYEKITI wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia amemtaka Rais Dk. John Pombe Magufuli kupeleka muswada bungeni katika kikao kijacho cha Bunge ili kuandaa sheria ya kuvifuta vyama vyote vya siasa na kuangalia kile ambacho yeye anaona kitafaaa kuiongoza serikali bila migogoro kama inayojitokeza sasa. Hayo ameyasema leo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Ilala-Bungoni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari. Mbatia alisema kuwa, Rais Magufuli hawezi kukinzana na upinzani uliopo kwa sasa kwa kuzuia mikutano na maandamano wanayotaka kufanya kwa kuwa yanak

Mfanyabiashara Ataka Kujirusha Daraja la Ubungo

Image
    Shayo akiwa juu ya daraja. Gari la Jeshi la Zima Moto likiwa eneo hilo. Baadhi ya wananchi wakimshangaa Shayo (hayupo pichani). Shayo akiwa anavutwa baada ya kumpa mkono ndugu yake. Akiwa anapelekwa Kituo cha Polisi cha Ubungo. Katibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha, akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa haki. Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha. Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni Mtanzania anahitaji haki ndipo walimsubiria al

Breaking News: UKAWA Wakubali Kurudi Bungeni Baada ya Mkutano na Viongozi wa Dini

Image
  Vyama vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF na ACT Wazalendo ambavyo vilisusia vikao vya bunge vimekubali kurejea bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini hapo jana

Zitto Kabwe afunguka yake kuhusu Oparesheni UKUTA

Image
  Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba. “Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hata hivyo, vikao vya maridhiano vinavy

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wi