SIRI NZITO YAFICHUKA MTANZANIA ALIYEWEKWA REHANI PAKISTAN,MKE AHAMISHWA NA JUMA,APANGIWA NYUMBA
NI mateso. Ndivyo unavyoweza kusema, hasa baada ya kundi la maharamia linalojishughulisha na bishara ya ‘unga’ nchini Pakistan kuelezwa kumtesa kijana Mtanzania, Adamu Akida. Kutokana na hali hiyo, timu ya MTANZANIA ilipiga kambi jana katika eneo la Magomeni, Mtaa wa Idrissa, ambako pamoja na mambo mengine, ilifanikiwa kuzungumza na kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi). Akisimulia mkasa huo, alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu. Baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa. “Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili ha...