Watuhumiwa wa ugaidi waigomea mahakama
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014. Wakizungumza leo mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao. Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa. Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi hewa na mkuu wa upelelezi kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi. Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu