Uwoya awawashia moto wanaomsakama kuhusu Dogo Janja
Mwanamama wa tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Uwoya amejikuta akiwaka baada ya kuhojiwa sababu za kutomposti mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya ambaye inadaiwa kuwa hayuko sawa na mumewe huyo alidai kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi. “Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya,” alisema Uwoya akionekana kuna jambo haliko sawa. Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake. “Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone,” alisema Uwoya