Posts

Showing posts from March 1, 2017

IRENE UWOYA AMLIPUA WEMA SEPETU NA WENZAKE,AWAPA MAKAVU LIVE

Image
Baada ya kashikashi za hapa na pale ya wasanii wa bongo movie kuingia kwenye siasa huku Wema Sepetu akihamia CHADEMA na kusema anaidai CCM, swahiba wake, Batuli amekanusha. Wakati vita vya maneno vikiendelea, mwenzao, Irene Uwoya amewachana. Irene ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno yenye busara ndani: Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana.” Mfano mim ni CCM da...

WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za Mvomero, Morogoro manispaa na Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na pikipiki maarufu kama boda boda. Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana na dawa hizo, wamekuwa na majibu tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo ...

ALLY KIBA APOKEWA KISHUJAA, AISIMAMISHA JIJI LA DAR ES SALAAM NA VIUNGA VYAKE

Image
 Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika                  Mashabiki wa AlyKiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani  Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake  Aly Kiba akiwa na Meneja wake  Seven Mosha mara baa da ya kuingia katika gari hiyo maaalum  Ally Kiba akiwa katika mitaa ya Kariakoo huku akiwa amezunguskwa na mashabiki mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona Tunzo yake ya Mtv base kama msanii bora wa kiume ...