Posts

Showing posts from December 30, 2013

ANGALIA NAFASI ZA KAZI LEO

Image
Sales Person Jason & Co Ltd. Date Listed:  Dec 27, 2013 Email Address:   Click to Email Phone:  No Calls Please Area:  Dar Es Salaam Application Deadline:  Jan 20, 2014 Position Description:   Click Here Application Instructions: Please send Applications to the Email Link above Yard Controller Mukuba Depot Date Listed:  Dec 27, 2013 Phone:  No Calls Please Area:  Dar Es Salaam Application Deadline:  Jan 10, 2014 Position Description: From Daily News December 27, 2013 MOFED  Tanzania Limited is a Freight and Forwarding service provider wholly owned by the Government of the Republic of Zambia under the Ministry of Transport, Works, Supply and Communications in lusaka  Zambia. It is based in the  Kurasini  Area next to the Dock Yard in Dar  es  Salaam. MOFED  Tanzania Limited is hereby inviting applications from suitably qu...

MTANZANIA HUYU KATAJWA KUWA NI MOJA YA WANAWAKE WAREMBO ZAIDI BARANI AFRIKA..!!

Image
Jarida la Glitz Africa limetoa orodha ya wasichana 20 warembo zaidi barani Afrika (20 Most Beautiful Women in Africa) ambapo hata hivyo imetawaliwa na wanawake wa Nigeria na Ghana. Ni Happiness Millen Magese pekee amekuwa mwanamke kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuingia kwenye orodha hiyo. Orodha nzima ni hii: Leila Lopes (Angola), Vimbai Mutinhiri (Zimbabwe), Oluchi Orlandi (Nigeria), Yvonne Nelson (Ghana), Dillish Mathews (Namibia), Agbani Darego (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria), Stephanie Linus (Nigeria), Genevieve Nnaji (Nigeria), Joselyn Dumas (Ghana), Yvonne Okoro (Ghana), Jackie Appiah (Ghana), Millen Magese (Tanzania), Omotola. Jalade-Ekeinde (Nigeria), Zainab Sheriff (Sierra Leone), Naa Okailey Shooter (Ghana), Nadia Buari (Ghana), Lerato “Lira” Molapo (South Africa), Babalwa “Barbz” Mneno (South Africa), Elham Wagdi (Egypt).

RASIMU YA KATIBA INAWASILISHWA RASMI KWA MHE RAISI JAKAYA KIKWETE,SOMA BAADHI YA VITU VILIVYOMO HAPA

Image
Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza ina ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240  -wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora -lugha ya kiswahili lugha ya taifa. -Madaraka ya Rais yamepunguzwa. -wabunge wasiwe mawaziri -kuwe na ukomo wa wabunge -wananchi wawajibishe wabunge  -spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa. -kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa. MUUNGANO 39000 walitoa maoni kuhusu muungano Tanzania Bara,na karibu wote wa Zanzibar walitoa maoni kuhusu muungano -Taasisi nyingi zilipendekeza serikali tatu. Malalamiko upande wa zanzibar Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania -mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka -kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais Malalamiko Tanzania Bara. -Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano -Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar Mambo mengi y...

TASWIRA KUTOKA KARIMJEE KATIKA MAKABIDHIANO YA RASIMU YA PILI KATIBA MPYA

Image
PICHA NA JULIUS S. MTATIRO

SNURA: WEMA NDIYO ALIYENITOA KIMUZIKI

Image
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ‘Mama Majanga’ ametoa ya moyoni na kumshukuru aliyekuwa rafiki yake wa damu, Wema Sepetu kwa kuwa ndiye aliyembunia vazi la muziki na fedha ya kurekodi wimbo wake wa kwanza. Snura Mushi ‘Mama Majanga’. Wema Sepetu. Akistorisha na paparazi wetu, Snura alisema fedha ya Wema ilihusika kumtoa kimuziki kwani wakati akirekodi wimbo wake wa kwanza, sauti yake iliingia kwenye wimbo huo na vazi lake la shoo ya kwanza alilibuni Wema ambapo mpaka sasa analiendeleza, hivyo anamshukuru sana na anamuombea kwa Mungu ambariki zaidi. “Namshukuru Wema, kwani alihusika sana kwenye wimbo wangu wa kwanza wa ‘Shogaake Mama’ kwani fedha yake ndiyo ilitumika kurekodi wimbo huo pia aliingiza sauti yake kwenye wimbo huo, alinibunia vazi la shoo yangu ya kwanza ambalo ninaliendeleza mpaka sasa,” alisema Snura.

KATIBU TFF AKATAA FEDHA ZA MATAJIRI WA SIMBA, YANGA

Image
KATIBU Mkuu mpya wa TFF, Selestine Mwesigwa ameingia ofisini na mkakati ambao hakuna tajiri yeyote wa Simba wala Yanga atataka kuusikia. Kama mkakati huo utafanya kazi hakuna fedha zozote za mashabiki au wanachama matajiri zitatumika kufanya vurugu za usajili, jambo ambalo huenda likashitua wengi. Yanga na Simba zimekuwa zikifanyiana vurugu kwa kupokonyana wachezaji wakati wa usajili huku wanachama matajiri ambao wengine si viongozi wakitaka kutunishiana ubabe na kuonyeshana nani mwenye fungu. Lakini Mwesigwa ameingia TFF na mfumo ambao utazizuia klabu kutumia fedha yoyote ambayo haitokani na soka kama zilivyozowea kufanya Simba na Yanga ambazo hazina vyanzo maalum vya mapato. Kwa mujibu wa Mwesigwa klabu zote za Ligi Kuu Bara zitatakiwa kujihadhari na matumizi ya fedha ambazo hazitokani na soka katika matumizi yake mbalimbali ikiwemo usajili. Mwesigwa aliliambia Mwanaspoti kwamba, moja ya mambo ambayo atayasimamia ni utekelezaji wa azimio la ...

WABUNGE 15 MATATANI

Image
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.  Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao. Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe. Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia. "Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini," alisema Dk Kashililah na kuongeza. Akizungumzia safari ya Kion...

JOKATE AWACHAMBUA MADEMU WENZIE

Image
Jokate Mwegelo aka Kidoti ana mengi ambayo ameyasoma kwa baadhi ya wasichana wa Tanzania na yeye akiwa mmoja wao na hivyo amezikusanya sifa hizo kama sampuli na kueleza kile anachokipenda na asichokipenda. Kama mrimbwende amewasifia wasichana wa Tanzania kwa jinsi wanavyojua kuweka sawa na kupendeza. “kitu ambacho nakipenda, napenda kwa sababu wanapendeza, wanapenda like..kupendeza, wanajitunza vizuri.” Jokate amefunguka kupitia The Switch ya 100.5 Times Fm. Lakini kwa upande wa kile ambacho anaona hakiko sawa, uvivu ndio anaoupigia mstari. “Kitu ambacho sikipendi, ni kwamba…yaani sijui niseme kwamba hawajitumi sanaa. Yaani bado sijaona njaa ile.” Amesema Jokate. “Kwa mfano ukiangalia kwa mfano Marekani sasa hivi, all top artists ni wasichana, kwa hiyo females wanahustle. Wasichana wakibongo tumezoea sijui kupewapewa au kutafuta kupitia njia za kimkatomkato. That’s a thing ambacho mimi sikipendi na sitakiappreciate maisha yangu yote.” Amefunguka Kidoti. Amefunguka...

PICHAZ...MMH..HATARI TUPU..SHINDANO YA KUMTAFUTA MREMBO ANAYEVUTIA KIMAHABA UKO USA LILIIVOKUA.

Image
CREDIT-KANDILI YETU

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AHUDHURIA JUBILEI YA KANISA KATOLIKI ARUSHA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kaisa Katoliki baada ya Ibada ya Jubilei ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha  iliyofanyika mjini Arusha  Desemba 30,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

MTANGAZAJI WA CLOUDS FM ADAM MCHOMVU ANALIMA BANGI LIVE

Image

KATIBA: MWELEKEO MPYA KUJULIKANA LEO

Image
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakitia saini Rasimu ya Pili ya Katiba juzi. Rasimu hiyo itakabidhiwa leo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein, Karimjee, Dar es Salaam. Picha ya mtandao.  Dar es Salaam. Swali la nini kilichomo katika Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya litajibiwa leo wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakapokabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein. Rasimu inayosubiriwa kwa hamu na wananchi wa kada zote itatolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo ilijadiliwa na kuboreshwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyoketi kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, mwaka huu. Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotangazwa Juni 4, mwaka huu. Hafla ya kukabidhi rasimu hiyo itafanyika leo saa 6.00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi m...